Walimu wakuu wazuiwa kuandikisha watoto wa darasa la kwanza

Atongwele

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
2,470
Reaction score
106
NAIBU Waziri wa Elimu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassimu Majaliwa, amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za msingi.


Majaliwa aliyasema hayo juzi, wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari na baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu mkoani hapa,katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.

Alisema watendaji wa vijiji ndio wanawafahamu zaidi watoto wanaostahili kuanza elimu ya awali na msingi kuliko walimu wakuu wa shule za msingi katika maeneo husika. Alisema kutokana na ukweli huo, kazi ya uandikishaji watoto wenye sifa ya kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, ni watendaji wa vijiji na kazi hiyo,itakuwa na ufanisi mkubwa kuliko kipindi cha miaka ya nyuma.

“Kwa hiyo, kuanzia sasa kazi ya kuanza kuandikisha wanafunzi wa madarasa ya awali na ya msingi, itaanza mapema mara tu shule zitakapofunguliwa Januari na hadi kufikia Agosti ya mwaka husika, kazi hiyo itakuwa imekamilika.Kwa sasa hatutasubiri hadi mwishoni mwa mwaka kuandikisha wanafunzi”, alifafanua Majaliwa.


Aidha, Naibu Waziri huyo, alisema kuwa kila mtendaji wa kijiji, anapaswa kuwakilisha ripoti ya kazi ya uandikishaji wanafunzi wa shule za awali na wale wa msingi mbele ya Kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC),ili kupata Baraka ya kikao hicho.Alisema ili kuipa umuhimu mkubwa elimu ya awali, ni lazima kuwepo na bajeti ambazo zitaonyesha ongezeko la shule za awali.

Katika hatuna nyingine, naibu waziri huyo alikumbusha kuwa kila shule ya msingi, ni lazima iwe na vyumba vya kutosha vya madarasa ya awali. “Wanafunzi wa shule za awali sio walundikwe tu madarasa au wawe wa kucheza tu kipindi chote wawapo shuleni, hapana, ihakikishwe wanasoma kikamilifu ili wakianza darasa la kwanza katika shule za msingi, wawe wameiva barabara,” alisema Majaliwa.




source: Mwananchi Communication Ltd

wadau hebu tujadili Agizo hilo la Naibu Waziri. Mimi naamini kuwa dhamira yake ni thabiti na lengo ni kupunguza matatizo yanayotokea wakati wa zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa shule za awali na msingi. Lakini pia inanipa ugumu hasa kwa maeneo ya mjini ambako baadhi ya wakazi wake hawana makazi ya kudumu. kama watoto wanaandikishwa kwa kigezo cha kujulikana, je kwa wale wanaohamia kwenye mitaa mingine wakati wa zoezi la uandikishaji wataandikishwa kweli watoto wao? Ikumbukwe kuwa zoezi la uandikishaji hufanyika mwishoni mwa mwaka kipindi ambacho wazazi wengi pia wanakuwa na pilika za kuhama kutoka mtaa mmoja hadi mwingine
 
Halafu hofu yangu mimi ni hao watendaji! wana utendaji kweli? kama unahitaji barua tu ya kupata aidha dhamana mahakamani au ufadhili wa mtoto yatima shuleni inakuwa na longo kibao, hapo siyo pande la kunyanyasa wananchi kwa kutoa kitu kidogo? haikuji kabsaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…