Katika utafiti nilioufanya kuanzia Julai 31 hadi sasa nimegundua makundi matatu ya walimu waliokataa kuunga mkono mgomo na sababu zao. KUNDI la kwanza ni la walimu walioajiriwa Februari 2012. Hawa wanaogopa kugoma kwa sababu wengi wao bado hawana uzoefu na bado si wanachama wa CWT. KUNDI la pili ni la wale wanaokaribia kustaafu. Hawa wanahofia kupoteza mafao ya kustaafu(pension) endapo serikali itawafukuza waliogoma. KUNDI la tatu ni la wale wanaopandishwa vyeo kiholela. Hawa wanatafuta kupanda madaraja hivyo mishahara ya kuongezeka.
Mgomo huu hauna tija kwa TAIFA.
Ni halali waalimu walio kataa kuunga mkono mgomo. Kila njiwa huruka kwa bawa lake mwenyewe. tusifuate mkumbo. wengine kesho wanahamia ofisi nyingine!! shauri yao wanao goma.
Asee wewe unaonekana kutumia kichwa chako kufuga nywele tu, emancipate your self from mental slaveryNi halali waalimu walio kataa kuunga mkono mgomo. Kila njiwa huruka kwa bawa lake mwenyewe. tusifuate mkumbo. wengine kesho wanahamia ofisi nyingine!! shauri yao wanao goma.
Hili ni kundi kubwa tu la wake wa viongozi wa serikali mkoani na wilayani. Mfano Mkuu wa Mkoa/Wilaya, Afisa tawala Mkoa/Wilaya, Maafisa Elimu/Kilimo/Biashara wa Mikoa/Wilaya na wateule wengine. Hili kundi linaathiri hata walimu wengine kwenye hizo shule na ninadhani huwa hawana madai ya muda mrefu maana waume zao huwashughulikia kwa kutumia madaraka yao.Mkuu umesahau wake za wakuu wa wilaya.