Walimu wamepoteza heshima yao kwa jamii. Wamekalia madai tu.

Dr Ntinkutina.

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2013
Posts
309
Reaction score
55
Kama kuna kitu kinachoumiza wazazi wa wanafunzi kwa sasa basi ni tabia ya walimu kukalia madai tu.
Mfano walimu walioajiriwa mwaka huu kati yao zaidi ya elfu 12 inasemekana hawajaripoti walikopangwa. Hapo heshima itoke wapi?. Hao vijana waliishambulia serikali toka mwishoni mwa mwaka jana kwa nini hawapangiwi vituo vya kazi?.
Walimu wakati madai yao mengine yakiendelea kushugulikiwa waache kulalamika, sijui mimi ni "graduate" siwezi fundisha kijijini!. Watambue kuwa hayati baba wa taifa alifundisha "Pugu" akiwa na M A (Hist& Econ) ya Uskochi, keep in mind mwl. was very smart, lakini alifundisha tena it was in 1950s. Sasa ninyi wa 2010s wenye cheti,diploma na 1st degree mnagoma kweli kuripoti? Mlikuwa hamjui kuwa shule nyingi za msingi na sekondari zipo vijijini?. Na nafikiri wengi mnatokea huko. Heshima itoke wapi?. Wapendwa wahurumieni wadogo zenu wenye tatizo kubwa la upungufu wa walimu!
 
Mazingira ya huko katika hizo shule za vijijini unayajua? Ni afadhali hata miaka ile ukimaliza chuo chochote baada ya F4 unaenda JKT kupata mafunzo ya uvumilivu, ubunifu na ukakamavu ili ukipangwa kijijini ukapambane na mazingira utakayoyakuta.
 
Walidanganywa wakifanya hujuma zero zikiongezeka Nchi isingetawalika kwa hiyo kale ka NGO kangepewa dhamana ya uongozi!
 
We umewah kufika maeneo watu wanakopangiwa?sehemu haina network,maji,umeme wala nyumba ya kukaa walimu.mfano mdogo nenda segala(kata ya itiso) halmashaur ya chamwino-dodoma.mazingira kama hayo unaishi vp?
 
we ndo bonge la kilaza,thea4 wakishaenda bila kupewa chao watakula kwa baba ako?acha hzo nchemba,katafute kura jmboni kwako kwa wasioelewa..Mwehu wee
 
we ndo bonge la kilaza,thea4 wakishaenda bila kupewa chao watakula kwa baba ako?acha hzo nchemba,katafute kura jmboni kwako kwa wasioelewa..Mwehu wee

Pesa za kujikimu zilipelekwa kitambo tu. Na kwa walioripoti wameisha ingizwa kwenye pay roll. Vijana wawe wazalendo.
Hapa Nchemba ameingiaje?. My friend, use your brain to think, how We can help this country? Our God created human brain with 14 billion cells, which can help us to think. Kwa upungufu wa walimu tulionao idadi hiyo ambayo haijaripoti ni kubwa sana. Ukupewa ubongo kuita watu vilaza.Utilize to the maximum your bain power.Tafakari.
 
ww kinakuuma nn wakati kazi ni hiari ya mtu? kama unaumia peleka ndugu zako wakawe walimu ili nao waje waende vijijini
 
Mazingira ya huko katika hizo shule za vijijini unayajua? Ni afadhali hata miaka ile ukimaliza chuo chochote baada ya F4 unaenda JKT kupata mafunzo ya uvumilivu, ubunifu na ukakamavu ili ukipangwa kijijini ukapambane na mazingira utakayoyakuta.

Sawa, hawa jamaa ata wangepelekwa JKT, bado Taifa lingepata hasara. Lakini mbona wengi tu wanatoka vijijini then leo wanapatosa. Je ni kweli sisi kama taifa ni watu tusio na dira? Tunajiendea tu? Kama vile tumekuja duniani kudhurura tu?. Au ualimu ni taaluma ya stress?. Mbona wanatia aibu kiasi hiki?
 
Jamani walimu tuko tayari kwenda popote na tunawasikitikia sana wtt wa shule za serikali kwa sababu ya serikali yao kuto tekeleza madai yetu hvy inapelekea kuumia kwa taifa lijalo.
N:B TUNAOMBA SERIKALI ITEKELEZE MADAI YETU TUONE KAMA KUNA MTU HATAENDA SEHEMU ALIYOPANGIWA AU HATAFANYA KAZI KWA BIDII
 
Kwani umeambia wanadai pesa ya kujikimu tu.?hv unaujua ufisadi uliopo ktk halmashauri zetu?au umetumwa kuongea haya?mpeleke mkeo akafundishe kwa mkopo,acha kutania watu ww,unataka uafisa elm?
 
uzoefu wangu unaonesha elimu ya primary na sec ndio inayodharauliwa sana na serikali so kama mwalimu yupo vizuri kiuchumi au amepata kazi nyingine anayoona inalipa aende bush akafanye nini ,ila kama masikini kama mimi kijijini kunamuhusu mia kwa mia
 
Tatizo la mleta mada ameangalia upande mmoja tu,hivi unajua yaliyoko Halmashauri au unakurupuka tu?
 
uzoefu wangu unaonesha elimu ya primary na sec ndio inayodharauliwa sana na serikali so kama mwalimu yupo vizuri kiuchumi au amepata kazi nyingine anayoona inalipa aende bush akafanye nini ,ila kama masikini kama mimi kijijini kunamuhusu mia kwa mia

Umekuwa mkweli. Huo ndo ukweli wenyewe. Tuwambie hao wanaojiita "modern teachers" . Ualimu ni wito. Baadhi hawajaitwa katika taaluma hiyo iliyoheshimika sana miaka ya nyuma. Kwa sasa ualimu ni kundi la watu walojaa malalamiko. Mara wajitoe CWT! Inatupa wasiwasi hawa wajenzi wa taifa la kesho ni watu wa namna gani? Infact duniani kote wafanyakazi wana vyama vyao vya wafanyakazi. Hawa walimu wetu vipi? .Unajua dunia imebadilika sana. Miaka ya nyuma kidogo Cheti cha sheria ilikuwa ni sifa inayomwezesha mtu kuwa Primary Court Magistrate(PCM), lakini leo u PCM uwezi kuupata bila LLB. Dunia imebadilika sana na mabadiliko hayo yanawalazimisha wahitimu wa ualimu kutoka
UDSM, UDOM,TEKU,SAUT etc waende shule za kata ata kama wata kataa kata kata!. Lakini ukweli ndiyo huo. spleen una akili nyingi rafiki yangu.
 
kweli we ni mburula umeambiwa walimu wanadai fedha za kujikimu? acha kukurupuka kama una hurume mpeleke mkeo na ndugu zako wakafundishe me naona umetumwa au kuna ndugu yako ni gamba kakupa huo ujumbe uandike humu jf? unawakera watu wenye taaluma zao baba yako angefanya kazi kwa mkopo ungesoma wewe? acha use.....................................
 
Mazingira ya huko katika hizo shule za vijijini unayajua? Ni afadhali hata miaka ile ukimaliza chuo chochote baada ya F4 unaenda JKT kupata mafunzo ya uvumilivu, ubunifu na ukakamavu ili ukipangwa kijijini ukapambane na mazingira utakayoyakuta.

si hilo tu na myumba vyombo kila kitu unakuta ndani, huyo hajui kitu gamba tu hilooooooooooooo! hiloooooooo
 
si hilo tu na myumba vyombo kila kitu unakuta ndani, huyo hajui kitu gamba tu hilooooooooooooo! hiloooooooo

Wewe unaishi kijiji gani ambacho ulikuta nyumba na vyombo ndani ulipoenda kuripoti ktk shule uliyopangiwa?
 
Dr Ntinkutina.
Heshima itoke wapi?

Dr kwani unapata heshima gani kwenda kufanya kazi huko Muruvyagila Sekondari (iko Ngara mpakani na Burundi), huku mahitaji hayapatikani kabisa vikiwemo vitabu. Vitabu vya kufundishia ujinunulie mwenyewe kwa fedha zako za mfukoni. Wewe ni mkazi wa Liwale, nauli ya kufika huko ni zile za korosho mzee kauza kwa stakabadhi ghalani. Kwa nini nisibaki nyumbani tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…