Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Ukiangalia kwa jinsi mambo yanavyoenda utagundua walimu wamesusa. Wanasema kwa sasa wao wanasubiri tu mshahara uingie maisha yao yaendelee.
Wanasema Serikali haiwajali, Wazazi hawawajali wamekuwa wakiwakebehi na kuona wao ni watu waliochokwa na kila kitu.
Sasa wameamua nao kukaa pembeni kuangalia mchezo unavyochezwa. Wao si hawana akili?wao si walalahoi? Wao si hawajielewi? Basi sawa. Ingawa wanauliza kwa kushangaa kuwa hivi nani ana tatizo?
Mzazi ambaye anampeleka mtoto wake kwa hawa watu wenye mapungufu lukuki au wao? Walitegemea sasa wazazi muwafundishe watoto wenu majumbani mwenu.
Wanaendelea kuongea kwa uchungu kuwa haina shida....watakutana mbele kwa mbele. Na wanasikitika kuwa wanaowakebehi walimu na kuwatusi wengi ni walalahoi,choka mbaya. Ila wenye uwezo na elimu huwa heshimu na kuwataka sometimes hata wakawafundishie watoto wao majumbani mwao.
Lakini akina kajamba nani ndo wanaopiga hesabu mshahara wa mwalimu na kusema bora wawe boda boda. Wao wanasema sawa haina shida. Ngoja sasa wawafundishe watoto wenu jinsi ya kuwa bodaboda wazuri huko mbeleni.
Sasa walimu wamesema hawahangaiki na kufuatilia nidhamu, kufuatilia masomo wala kuhangaika na kitoto na litoto la mtu. Si wao wanapotaka waweka sawa watoto wenu ninyi mnakuja juu? Haina shida. Wataacha mitoto yenu itake ile mbaya. Watoto wa wazazi wanaojielewa watasoma. Wanasema miaka ijayo maji na mafuta yatajitenga tu.
Haya maneno nimeyapata toka kwa walimu zaidi ya 25 ambao nimeongea nao wakati nikifanya research. Mwezi ujao nitakuwa naongea na manesi,then madaktari. Kisha nitamalizia na watoto wenu (waendesha boda boda) kama ambavyo nimedokezwa na walimu wengi.