tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,133
- 280
Walimu mnaokwenda kujiendeleza katika vyuo vikuu na vyuo vingine mnapaswa kuomba ruhusa katika mamlaka husika. Bila kufanya hivyo, mtahesabiwa kama watoro kazini na hivyo kuiweka ajira yenu rehani. Naibu waziri wa Elimu Mh. Phillipo Mulugo atahakikisha kwamba utaratibu huo unazingatiwa.
Kwa uzoefu nilionao ni kwamba hata wale wanaoomba ruhusa wengine huwa wanatiliwa ngumu na wakubwa wao kuanzia kwa wakuu wa shule, maafisa elimu, wakurugenzi nk. Unaweza ukaambiwa shule ina mwalimu mmoja tu wa somo fulani sasa ukiondoka nani atafundisha au wewe hauko kwenye mpango mwaka huu na sababu nyinginezo.
Sasa ndugu zangu uamuzi ni wako: uende kusoma ajira ikome na ukihitimu uanze upya au ubaki shuleni usiende kusoma.