<br />
<br />
Wanasheria ndio kabisaa.unaweza ukafungua hata mahakama au chember court hapo nyumbani. Ni wajuaji sana kila kitu wanataka kiende kisheria sheria,ikiwezekana unapoongea uwe unafanya na citation kabisa.
Sijui kama ndo zao ni za kweli, ni kweli walimu (wakike) wanaongoza kwa kuolewa lakini kuna sababu, walimu wengi wa kike wanaolewa ili wapate nafasi ya kufundisha shule za mjini, mwl akifunga ndoa mara utamuona anaanza kutafuta uhamisho, nini? namfuata mume wangu, halafu ndoa zao nyingi ni za bomani, wachache sana wanaofunga ndoa za kidini (christian/islamic)
Mwana siri ni hii HUWA HAWAZEEKI(HAWACHUJI) UPESI
Pia msisahau kuwa wasichana wengi wazuri huwa hazichaji sana darasani kwahiyo wengi wao huishia kuwa walimu wa shule za msingi na sekondari kama amejivuta kidogo. Ukitaka kuthibitisha hili tembelea vyuo vya ualimu utafikiri wasichana wazuri walichujwa wakapelekwa huko.
aisee kweli wewe mchunguzi, lakini wengi wanaolewa kwa sababu ya kukimbia vijijini, maisha magumu huko