Walimu wapya Halmashauri ya Morogoro vijijini hawajalipwa Mishahara

chung cho

Senior Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
191
Reaction score
42
Jambo la kusikitisha sana mpaka saa hizi walimu wapya wa morogoro vijijini walioripoti tarehe 1 april mpaka 5 april hawajalipwa mishahara yao. kwa mujibu wa waziri tamisemi alisema wote walioripoti katika tarehe tajwa ndo waliolipwa mshahara katika hotuba yake bungeni lakini si hivyo kwa halmashauri hii ya morogoro vijijini mpaka sasa walimu wanakaribia kufa na njaa serekali tafadhali ingilieni kati juu ya jambo hili maana walimu wameanza kukosa uzalendo wa kuitumikia nchi yao na muda si mrefu maandamano na migomo inakaribia kuanza. Ole wenu mnaokula haki za walimu
 
Poleni waalimu. Dua la kuku halimpati mwewe, muache kuisaidia ccm wakati wa uchaguzi kufanya maasi.
 
Sleeping giant tena yaani maneno tele hamna vitendo.
 
Walimu hawa sio wa kuwaonea huruma wakome kwanza
 
Naona mafisadi mmeanza kucomment mkishamaliza wenye busara zao wataendelea kucomment. Sawa sawaaaaaa
 

Mkuu mbona hiki kilio cha waalim wapya kutolipwa kimetalamaki kila kona ya nchi kwa utukufu wa hali ya juu!!!!

Akichangia bunge maalum la katiba kwenye madai ya baadhi ya wabunge kudai laki3 hazitoshi, naibu waziri wa fedha ndg Nchemba aliwananga wabunge waliodai nyongeza kwamba kama wanaona laki3 hazitoshi waondoke, na kwamba serikali inahitaji fedha kulipa waalim wapya na huduma nyingine, sasa mbona hao waalim wanakufa njaa??

Hii nchi ngum sana!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 

Mkuu ninachoona walimu waanze kuingiza siasa mashuleni kwa kutoa elimu kwa wale form four au form five na six walio nao nao mashuleni kupigia kura vyama pinzani na kuwashauri wakawaelimishe na wazazi wao vivyo hivyo iwe mjini au vijijini najua kwa sasa vijana ndo wenye nchi na walimu najua mna ushawishi mkubwa mbele za wanafunzi hao ambao wengi wao wana umri wa miaka 18 na kuendelea.
 

Binadamu haishi kwa mkate au mmesahau, endeleeni kushaangilia CCM inatosha muendelee kuishi hela za nini nyie watu, tunakamilisha ufisadi wa 200Billlion tuko busy
 

Madai ya waalimu kuidai serikali hayajaanza Leo, ni wimbo ambao umerithishwa toka kipindi kimoja cha uongoz kwenda kingine. Leo hii tunaongelea madai ya mabilioni ya shilingi wanayodai waalim toka vipindi vya uongozi vilivyopita.

Najiuliza serikali hii ambayo inadeni kubwa sio tu kwa waalim bali hata watumishi wengine, inawezaje kuendelea kuajiri waalim au madaktari isiyoweza kulipa madeni ya mwanzo? Uliona wapi unaruhusiwa kukopa ilhali deni la mwanzo bado bichi!!!!!!

Majuzi tuliarifiwa kwamba serikali imepewa onyo na taasisi za fedha za kimataifa kwamba inakoelekea haitakopesheka kutokana na kuongezeka kwa deni; unastaajabishwa na taarifa kama hizo kwa kujiuliza pesa tunakopa lakini mbona matumiz hayaeleweki?

Serikali iachane na matumizi mabaya ya fedha, iwekeze kwenye kuboresha maslahali ya watumishi na miradi ya maendeleo, wakusanye kodi na sio kuruhusu wengine walipe wengine wasilipe,,

Ushauri wako kuhusu waalimu kuhubiri siasa za upinzani kwa mtazamo wangu mm naona bado hauna mashiko; ni kwa sababu serikali bado inadeni kubwa kwa watumishi wake wote, waalim, wanajeshi, madaktari, polisi nk.

Sasa hao wengine ukiondoa waalimu nani atakuwa balozi wao, nadhani watanzania wote kwa sasa inatosha kuburuzwa na serikali isiyojua nini wajibu wake,, mabadiliko ya mfumo wa uongozi kuanzia juu yanahitajika haraka sana.

Nawasilisha.


Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 
Kuna kazi ukifanya lazima upate matatizo.
 
Serikali yetu ya Tz bwana! Huku ulanga mambo ni magumu sana. Pesa ya kujikimu hatujapewa yote na mshahara wa mwezi hausomi, da!
 

uko shule gani?/ kiroka sec?
 
uko shule gani?/ kiroka sec?

Shule itakusaidia nini unachotakiwa watatulie walimu shida zao kama wewe muhusika maana walimu hawakupewa mishahara yao mpaka sasa kwamba yupo nelson mandela sec., ngerengere sec, mkuyuni sec, mikese sec, matombo au kiroka sec haitakusaidia cha msingi ni kulipwa mishahara ya mwez april.
 
vumilia mtalipwa hela zenu usipende kulalamika kama umejaza mkataba na kusaini haina shida tulia utalipwa.
 
vumilia mtalipwa hela zenu usipende kulalamika kama umejaza mkataba na kusaini haina shida tulia utalipwa.

Ndio muwalipe sio mnatutesea watoto wetu.sio mnawannyonya damu alafu mnataka waishi. Rudisheni uzalendo wa watu kuipenda nchi yao na kazi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…