Walimu wapya mnataka kuganga njaa au kulitumikia taifa?

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Takribani sasa miezi kadhaa imepita Serikali ilipotoa taarifa ya kuwapangia vituo vya kazi wahitimu wa fani ya Ualimu. nilitegemea wahusika kutochukulia maanani kauli hiyo maana wengi wao wanalaamika, wanahujumu watoto wetu kwa kutoingia madarasani, matokeo ya wanafunzi yakiwa mabaya wanashangilia...kwa ujumla naweza kusema hapa Tanzania kwasasa walimu wana mgomo barafu wakishinikiza serikali iwaongezee mshahara.

kwa mshutuko mkubwa kila kukicha walengwa hawa wanahaha kila kona kusaka ni lini watapangiwa nafasi hizo......hata hapa JF kuna post nyingi sana zinazouliza nafasi hizo.

Hivi nyinyi mnataka kulitumikia taifa kizalendo bila kujali hali iliyopo au ni njaa za mtaani ndio zinawasukuma hivyo.....Tafakari..... chukua hatua!
 
njaa zinawasumbua wakisharipoti wenyewe watakuwa wanrudi town na kutaka kuendelea na master na kutelekeza watoto wawakulima vijijin bila waalimu
 
Anyway,sijajua wewe mtoa mada mtazamo wako ni upi,ila kuna kitu (kwa mtazamo) nahisi umeteleza kidogo.Je,umejiuliza watu wanaoingia jeshi na kwenda vitani(wengine wanafia huko) wanafanya hivyo kwa sababu gani,je ni uzalendo au ni njaa yao? Na vipi wewe kama umeajiriwa ni kwa sababu ya njaa yako au uzalendo? Madaktari walipogoma na bado wanataka kuajiriwa,je wanafanya hivyo kwa njaa zao au ni uzalendo? Walimu wana matatizo mbalimbali,je tuondoe fani ya ualimu katika mfumo wetu ili kuepuka tatizo la waganga njaa?

Maswali mengi..... ambayo ulitakiwa kujiuliza na kupata majibu yake kabla hujapost hili wazo lako.
 
Sitaki kukuita kilaza ila hoja yako haina mashiko kajipange upya ndo uje huku jf tena
 
uzalendo ulishakufaga zamani...hapa ni chapaa uzalendo kwa wazazi wako....unaleta uzalendo wenzako wanazitafuna....kwani walimu wamekuwa Yesu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…