Walimu wapya tumesahaulika

Acha upumbavu kwenye mikataba yako ulijaza unaaanza unaanzia Tgts gani?! Ulichojaza kwenye mkataba ndio unachoanza nacho
Hakuna TGTS G7 kama ulivyosema na kumbuka mimi sio ajira mpya nipo kwenye gemu kitambo
 
Hongera dogo, ni kweli mmeanza na D3 walimu wa science?
 
Miezi miwili tu una lalamika wakati wenzako wanao anza kazi wana kaaga mpaka miezi 4..
 
Ole wenu mhamie private!

Tutawafutia vi degree vyenu na kutia kufuli vishule vilivyowapokea

Nasema Uongo Ndugu zangu?
 
Ole wenu mhamie private!

Tutawafutia vi degree vyenu na kutia kufuli vishule vilivyowapokea

Nasema Uongo Ndugu zangu?
Kweliiiii, hawa walimu wa siku hizi hawana uzalendo. Hata wakilipwaa hakuna anayeridhika na mshahara🤣
 
Kila mtu angevumilia na kuridhika hii dunia ingefika hapa ilipo? Kijana anadai haki zake nyie mnamletea busara zilizozeeka!
 
Serikali ya ajabu maana wenzenu walioajiriwa tangia 2014 wapo D1 hadi leo.
Hongera sana piga kazi
Hili tatizo limesababishwa na Nchi kuongozwa na mtu mmoja! Huku akijigeuza kuwa Alfa na Omega. Ni jambo linalo kera sana!

Yaani wafanyakazi walioajiriwa mwaka 2014 mpaka leo wako daraja lile lile! Halafu wanapo lalamika wanaishia kutishwa, kukejeliwa au kuletewa stori za kipuuzi puuzi tu mfano eti tunanunua ndege kwanza, subirini uhakiki upite kwanza, tumedhibiti mfumuko wa bei, kabla sijamaliza muda wangu nitaongeza!! Sasa hivyo vitu vina uhusiano gani na mfanyakazi kupanda daraja ambalo lipo kwa mujibu wa sheria na kanuni za kazi?

Hivi huyu mzee anafahamu kuwa ame/anawaumiza watumishi walio/wanao karibia kustaafu na wale wengine walio jiwekea mipango yao ya kimaendeleo?

Mtu alitakiwa astaafu na TGTS H mfano kwa walimu, lakini kutokana na huu uonevu wa kutopandishwa daraja unakuta mtu huyo huyo anastaafu na TGTS F!! Hivyo kujikuta akilipwa pensheni ya TGTS F badala ya ile halali ya TGTS H! Hapo achilia mbali wale aliwatumbua kwa kigezo cha vyeti feki huku wengine wakikaribia kabisa kustaafu!!

Rais Magufuli anawaumiza sana Watumishi wa Umma. Kama inawezekana, Mungu amuadhibu haraka kwa hizi dhambi zake anazo tufanyia tangu aingie madarakani mwaka 2015.
 
Daaah ni hatari hili waziri mwenye dhamana yuko kwenye nyungu daaah ncchi ya vituko sana
 
Hivi nikikosea kutuma ela nikatuma k8makosa naweza kuipata kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…