Walimu wapya wagoma kupokea fedha za kujikimu

Walimu wapya wagoma kupokea fedha za kujikimu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
na Stephano Mango, Songea


amka2.gif
WALIMU 52 wa Sekondari waliopangwa kuanza kazi kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamegoma kupokea fedha za kujikimu zilizotolewa na halmashauri hiyo kwa madai ya kuwa ni ndogo, tofauti na ilivyopangwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za halmashauri hiyo walimu hao ambao waliomba majina yao yahifadhiwe kwa kuhofia ajira zao, walieleza kuwa walianza kazi tangu Januari 24 mwaka huu wakiwa wamepangiwa na tayari wameshapangiwa shule za kufundisha lakini posho za kujikimu walikuwa hawajalipwa.
Walisema tangu waanze kazi wameishi katika mazingira magumu kwani hadi sasa wanadaiwa fedha kwenye nyumba za kulala wageni ambako wanaishi na huku wakiwa hawana uhakika wa kupata chakula.
Walisema kuwa halmashauri hiyo ilipangiwa walimu wa shule za sekondari 126 lakini waliokwisha kufika mpaka jana ni walimu 52 tu ambapo wapo wa stashahada na shahada.
Walibainisha kuwa walipofika katika halmashauri hiyo wahasibu walitaka kuwagawia fedha kati ya sh elfu 90 na laki 130,000 kwa maana kwamba walimu wa shahada walipaswa kulipwa shilingi 130,000 ambazo ni fedha za kujikimu kwa siku 2, jambo ambalo liliwafanya wagome kupokea fedha hizo kwa madai kuwa ni ndogo.
Walisema kuwa walipaswa kulipwa fedha za kujikimu kwa siku 14 na si mbili kama ilivyofanywa huku viongozi wa manispaa hiyo wakidai kuwa fedha ambazo zilitengwa kwa ajili ya posho za kujikimu hazijafika kutoka Hazina. Kwa upande wake Ofisa Elimu wa Sekondari, Hnji GodiGodi, alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na malalamiko hayo alieleza kuwa mpaka sasa fedha za kujikimu kwa walimu wapya waliopangiwa na Tamisemi bado hazijafika. Alisema kutokana na hali hiyo ofisi yake ililazimika kuchukua fungu la fedha za kuwalipa walimu wanaokwenda likizo Machi mwaka huu ili kuwalipa walimu hao lakini alishangazwa na hatua iliyofanywa na walimu hao kwa kuamua kugoma.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Dk. Anselm Tarimo alisema kuwa serikali ilitoa maelekezo juu ya walimu hao ambao wanapaswa kulipwa posho za kujikimu wakati wa kuanza kazi za siku 14 .








source Tanzania Daima
 
Mwaka huu naona mpaka watu waingie msituni, kila kona manungúniko!
 
Aisee hii kitu sio kwa waalimu pekee,bali ni watumishi wote wa ajira mpya na ni almost halmashauri zote.sijui ni waziri yupi anahusika.halafu unakuta serikali inabwata eti watumishi waliopangwa vituo vya kazi vya pembezoni hawafiki kumbe upuuzi ni kama huu.
 
Nchi hii kweli shamba la bibi.Hata MBOZI wanatikisa kiberiti.Wakurugenzi wanageuza ajira mpya kuwa deal la kuchakachua!!.Huu ndio mwisho wa serikali ya CCM,2015 hatuta kosea!
 
Back
Top Bottom