Walimu wasio na Ajira (NETO) waibua mazito yanayofanyika kwenye vituo vya usaili. Wataja rushwa na kukosa usawa

Walimu wasio na Ajira (NETO) waibua mazito yanayofanyika kwenye vituo vya usaili. Wataja rushwa na kukosa usawa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Umoja wa Waalimu Wasio na Ajira (NETO) wamefunguka sintofahamu ya ajira iliyopo kwa wahitimu kuanzia mwaka 2015 mpaka 2023.

Soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

Kwa upande wa masuala ya usaili wamedai "kumekuwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikituumiza wasailiwa, changamoto hizi ni kubwa zimefika hatua zina athiri mpaka uchumi wetu moja kwa moja wasailiwa ambao ndio tuna maisha magumu mtaani, hawana ajira wanajitafuta kwa kiwango kidogo sana na kupata lakini wameathiriwa na huu usaili, wametumia gharama kubwa sana kiasi hatua ambayo wengine wameingia madeni."

 
Pole yao kwa kweli....natamani kusikia majibu ya upande wa serikali.

Nacho jua ni kua waziri mkenda atawapuuza..

Kidogo hayati angekuwepo angelifanyia kazi na kutoa matamko Ila kwa Sasa mama yetu yupo busy na UCHAGUZI ujao so Hilo ndilo kipaumbele kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom