the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Umoja wa Walimu wasio na ajira nchini Tanzania (NETO), umemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan na Serikali, kuwasaidia Walimu hao kupata ajira na kuweka usimamizi madhubuti pamoja na kufuta mfumo wa usaili katika mchakato wa kutoa ajira.
Uongozi wa Umoja huo kupitia kwa Katibu wake Daniel Edgar mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, pia umeeleza kusikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya Viongozi wa Serikali kwamba Waalimu waliokaa muda mrefu bila kuajiriwa hawana ubora wa kutosha jambo ambalo wanalipinga na kusema kuwa sio kweli.
Pamoja na hayo, Katibu huyo ameomba Serikali kufuatilia Shule binafsi zilizopo Tanzania kwani wamegundua kuna Waalimu wenye degree wanalipwa mshahara wa shilingi laki moja na nusu huku wale wenye Diploma wakilipwa shilingi laki moja.
“Unakuja Shule ina Watoto 1200 na kila Mtoto analipa ada sh. milioni 1.2 lakini Mwalimu analipwa mshahara laki mbili laki tatu, tunaomba Serikali iingilie kwenye Sekta binafsi”