Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kuwapeleka walimu 10 wa shule za msingi na sekondari Dubai kwa watakaofanikisha ufaulu mwakani, imeonekana kuwaamsha walimu kila mmoja akiahidi kufundisha kwa bidii ili kupata nafasi hiyo.
Akizungumza leo Julai 16 katika kikao cha tathimini ya elimu mkoani humo kilichohusisha wadau wa sekta hiyo ikiwa ni kupongeza matokeo mazuri ya kidato ch sita yaliyotangazwa hivi karibuni, Homera amesema watatoa ofa kwa walimu 10 kwenda Dubai.
Amesema kutokana na matokeo mazuri yaliyopatikana mwaka huu, Dubai ndio sehemu nzuri kwa mapumziko akieleza kuwa ofa hiyo itahusisha walimu wa shule za Serikali huku za binafsi kamati itakaa kujadili zawadi.
Amesema kwa sasa Mbeya ipo katika ramani nzuri kielimu, inazidiwa na mkoa mmoja tu (hajautaja) akieleza kuwa mkakati ni kushika nafasi ya kwanza akiwatia moyo walimu kuwa inawezekana.
"Wakati nafika hapa Mbeya tulikuwa nafasi hazijulikani, lakini kwa sasa matokeo yetu hayana sifuli, tuna daraja la kwanza 4,047, la pili 2726 daraja la tatu 487 na nne ni tano, niwapongeze walimu kwa kazi nzuri.
"Niagize kila halmashauri yenye uwezo inaweza kuwapa zawadi shule zilizofanya vizuri na mwakani walimu 10 ikiwa watano shule za msingi na watano sekondari tutawapeleka Dubai katika hoteli ya nyota tano wakirudi wawe wamebadilika kwa kuongea Kiingereza," amesema Homera.