BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Walimu wa Shule ya Msingi za Kishinda na Isebya zilizoko kata ya Kishinda wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wanatuhumiwa kupora vifaa vya wanafunzi baada ya kumaliza mtihani wa kitaifa wa darasa la saba. Malalamiko ya wahitimu hao yaliwasilishwa na Diwani wa Kata ya Kishinda, Shokolo Visent kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kilichofanyika Oktoba 28 na kuwaamuru walimu hao kulejesha vifaa.
Walianisha vifaa hivyo kuwa kilamu za wino, peseli, vichongeo pamoja na vifutio ambavyo vilinunuliwa na wazazi wa wanafunzi hao na siyo mali ya shule. "Ingekuwa mali ya shule vingebaki shuleni lakini kwa sasa siyo mali za shule vifaa hivyo vinatakiwa walejeshewe wanafunzi, amesema Shokolo.
Kutoka na malalamiko hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga amesema walimu hawana mamlaka ya kuwanyang’anya wanafunzi vifaa vyao baada ya kumaliza mitihani yao, hivyo ameamuru vifaa hivyo vilejeshwe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Binuru Shekidele amesema atafuatilia suala hilo ili abaini ukweli wake na kuwataka walimu waliochukua vifaa hivyo wavilejeshe kwa wenyewe. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kishinda, Raymondo Alex amesema ni kweli vifaa hivyo vilikuwa vimekusanywa na ilitokana na makubaliano kati ya wahitimu hao na mwalimu wa darasa lao.
Lakini kutokana na maagizo hayo vifaa hivyo vimerejeshwa kwa wahitimu hao ili kuondoa mkanganyiko huo.
MWANANCHI