Walimu wenye somo moja la kufundishia wataajiriwa?

Walimu wenye somo moja la kufundishia wataajiriwa?

Joined
Jan 15, 2015
Posts
67
Reaction score
8
enyi wana jamv kuna kajambo fulan kananitatiza mwenzenu mpaka nakosa raha yaan hapa maskan kuna mdogo wang kasoma psychology na somo moja la kifundishia la kiswahili pale TEKU na je kwenye ajira za mwaka huu anaweza akaajiriwa?mnisaidie kwa mawazo wadau
 
enyi wana jamv kuna kajambo fulan kananitatiza mwenzenu mpaka nakosa raha yaan hapa maskan kuna mdogo wang kasoma psychology na somo moja la kifundishia la kiswahili pale TEKU na je kwenye ajira za mwaka huu anaweza akaajiriwa?mnisaidie kwa mawazo wadau

Huyo si mwalimu wa sec,atafundisha diploma kama atapata baati,
 
mm mbona wapo wengi tu wanafundisha sec.usimkatishe tamaa mwenzio tena uwa wanakua wakwanza kwenye ajira.
 
SERIKALI imesema ajira za walimu wapya
zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu huku
ikiweka wazi kuwa walimu hao wasitegemee
kupangiwa katika maeneo ya majiji,
manispaa na miji.
Walimu hao wametakiwa kutotegemea
kupangiwa katika maeneo hayo kutokana na
idadi ya walimu waliopo ni kubwa na inakidhi
mahitaji, huku maeneo yaliyopewa
kipaumbele ni vijijini na halmashauri ambazo
zina mahitaji na upungufu mkubwa wa
walimu.
Idadi ya walimu wapya watakaoanza ajira
zao mwezi ujao ni 31,056 ambapo kwa
walimu wa ngazi ya Cheti ni 11,795,
Stashahada (Diploma) 6,596 na wenye
Shahada (Degree) 12,665.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
ajira mpya za walimu kwa mwaka
2014/2015.
Alisema kwa mwaka huu ajira hizo
zimechelewa kutokana na TAMISEMI pamoja
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
kufanya ufuatiliaji wa kina hadi katika ngazi
ya shule ili kubaini kwa uhakika mahitaji
halisi ya walimu kwa kila halmahauri na
shule.
“Ufuatiliaji huo umebaini kuwepo kwa
halmashauri na shule hasa za mjini zenye
walimu wa ziada na zingine hasa za vijijini
zina upungufu mkubwa wa walimu,” alisema
Sagini.
Alisema taarifa hizo zimesaidia kuwapanga
walimu wapya kwa usawa ili kuondoa
uwiano usioridhisha kwenye maeneo mengi
ya vijijini. Alisema kwa sasa wanakamilisha
taratibu za kupata kibali kwa ajili ya ajira za
walimu na fedha za kuwalipa stahili zao ili
waanze ajira zao rasmi mwezi ujao.
Aidha, alisema orodha ya walimu na vituo
watakavyopangiwa vitawekwa katika tovuti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambayo
ni www.pmoralg.com na ya Wizara ya Elimu
www.moe. go.tz ifikapo Aprili 24, mwaka
huu.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa
TAMISEMI, Zuberi Samataba alisema, pia
ufuatiliaji huo ulikuwa ni kuhakikisha
wanakuwa na taarifa sahihi za walimu
wanaoajiri wote ni wapya ambao
hawajawahi kuajiriwa ili kuepuka usumbufu
kwa walimu ambao hawatoi taarifa.
Alisema baadhi ya walimu ambao
wameshaajiriwa wanapoenda kusoma,
hupangiwa upya vituo na hawatoi taarifa
hivyo kuleta usumbufu wa kuchelewa
kutopata mishahara yao.
“Kuna baadhi ya walimu wameshaajiriwa
kwa hiyo jina linapoingizwa katika taratibu
za malipo, linagoma kuingia ndipo ukifuatilia
unajua alikuwa ameajiriwa, inabidi
umwambie arudi kwa mwajiri wake.
Kwa hiyo kwa hawa walimu wapya
nawashauri waende kuripoti katika vituo
walivyopangiwa na wakubali kufanya kazi
katika maeneo hayo, sio waripoti halafu
waondoke,” alisema.
 
Labda tu itokee bahati mbaya mwaka huu lakini wengi tu wa hivyo wamepata kwa mf. mwakajna kuna mtu alisoma philosophy and literature alipangiw kituo kam mwl wa literature!
 
watapata coz hata mimi nina jamaa zangu kibao walisoma philosophy na somo moja la kufundishia na walipangiwa na wapo waliopata bahati wakapelekwa vyuo vya ualimu!
 
Back
Top Bottom