Walinikatisha tamaa, gari hii nikajasiri ni bomba sana

Njele

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
275
Reaction score
121


Kama ni kukatishana tamaa basi, sikutaka kukubali kutokana na sifa ambazo baadhi walio na vyombo hivi wanivyonishawishi.

Niliagiza nikaipata, ni gari nzuri, inapanda milima, inapasua tope, inapenya mchanga, madimbwi ya maji hayafui dafu. na kabisa ni 4wd. Utaipenda.

Halafu kwa wese usiombe, very very economy. Kwa wanaotaka magari ya kujionyesha waendelee na yao, lakini wa kiwango changu ya kuendea kazini ni poa sana.
 

Tupo watu wa aina nyingi mno hapa, wale wenye mapenzi mema na wale wenye mchanganyiko wa mengi, bora kuomba ushauri kwa watu fulani watumiaji wa chombo hicho kuliko kumwaga mahala kama hapa wengi wamekatishwa tamaa katika mangi ingawa kuna washauri wazuri wengi tu.

Unapoomba ushauri mahala kama hapa nitahidi kuchambua ngano na ndago, yote ukiyatilia maanani hatima utayajutia.

Aina ya gari kama hii ningali na kumbukumbu ya ile Suzuki Samurai, ilikuwa nzuri, inapenya kila hali ya mazingira ingawa kwa umbo ilionekana ndogo. Gari hizi zimetengenezwa kwa matumizi ya mazingiara magumu. Hongera kwa kufanikisha na pia funzo kwa wengi.
 
Mkuu naitaka sana hiyo gari hebu nipe breakdown ni ya mwaka gani, imekugharimu kiasi gani kuanzia kununua mpaka kuitoa bandarini?
 
Njele. Hongera sana kwa kusikiliza roho yako. Mimi ninako na kwa kweli nimekakakubali mpaka sasa. Mafuta, kananusa tu.
 
 
Daah mkuu, are you sure? premio cc kubwa sijani kama inaweza kula 15km per litre, ni 10-12per litre haiwezi kuzidi hapa, vitz sawa but not premio, hebu check vizuri mkuu
 
Daah mkuu, are you sure? premio cc kubwa sijani kama inaweza kula 15km per litre, ni 10-12per litre haiwezi kuzidi hapa, vitz sawa but not premio, hebu check vizuri mkuu
Ni typing error Mkuu, nime edit. Ni 13Km per litre na ina CC 1580
 
 
Njele. Hongera sana kwa kusikiliza roho yako. Mimi ninako na kwa kweli nimekakakubali mpaka sasa. Mafuta, kananusa tu.

Nilitafuta gari hiyo kwa matumizi tu ninapokuwa likizoni nyumbani, kwani huku ninakoishi niliona gari hiyo imeingia miezi michache toka Japan na wazungu wanaichangamkia sana tu, na maelezo ya fuel economy ndiyo mpango kamili walivyoniambia. Nimejaribu ni bora kuliko gari ambalo unajaza mafuta unashtukia kama kuna shimo linalovujisha. Wengi wanaondokana na haya magari makubwa kutokana na mafuta yalivyo ghali siku hizi.
 
Mkuu naitaka sana hiyo gari hebu nipe breakdown ni ya mwaka gani, imekugharimu kiasi gani kuanzia kununua mpaka kuitoa bandarini?

Sikununua mpya, ni used, 2005 ambayo iko ndani ya limit ya imported care Tanzania bila tozo la extral. Niliipata ikiwa na 65,000Km, yaonekana kama mpya kabisa. Na ndugu yangu anafanya kazi ya dealership huko ndiye aliyenifanyia uhakiki wa gari maana kununua mtandaoni tu unaweza kushtukia unaletea gari ambayo siku chache unahitaji kumpelekea fundi.

Gharama za kununua, inspection na shipping hadi Dar $3,700. Bei inategemea na magari yalivyo sokoni.

CC; Bulldog
 

Njele: Hiyo gari Suzuki Swift ni nzuri sana, na nakupongeza kwa uchaguzi wako! Kuna jamaa yangu aliinunua 2009 inadunda mpaka leo, na inatumia mafuta kidogo mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…