Kumbe kurudia kusahihisha ndiyo "hufaulisha",
Kusoma miaka mi-4 shule ina Mwalimu mmoja ndiyo kunatatuliwa na kuridwa kusahisha?
Kujaziwa Zombie kwenye answer sheet kunabadilika na kuwa majibu sahihi unaporudia kusahihisha mitihani?
Ninaogopa tusijekutafuta "chambio" likasababisha kupeleka Kidato cha Tano watoto ambao hata hawajui Tanzania ni Muunganiko wa nchi ipi na ipi
Kuna tatizo kubwa ambalo linahitaji akili zilizotulia na zilizona dhamira ya dhati kulishughulikia na sio kurudia kusahihisha mitihani....Kuna tatizo kubwa zaidi ya usahihishaji na grading....na sio kwamba hawajui, upuuzi umejaa unaotaka kutuharibia watoto wetu na mustakabali mzima wa elimu yetu pamoja na Tanzania yetu katika ujumla wake....Watoto hawafundishwi, wanachojua ni soka la kina Messi na Mazombie leo unataka kuniambia kusahihisha mitihani pekee kutatosha?
Huu ni ujinga mwingine uliowekwa kwenye ganda la "chocolate"