Walioanzisha kodi leo wanaziita kandamizi na kuagiza zifutwe

Walioanzisha kodi leo wanaziita kandamizi na kuagiza zifutwe

Mzalendo120

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
2,410
Nimeona gazeti la Habari Leo la tar. 05/03/2023 na kichwa cha habari. "CCM WAAGIZA KODI KANDAMIZI KUFUTWA"

Nimetafakari na kuhitimisha kwamba aidha watanzania wanachezewa akili au hao wahubiri kuna mahali wanapwaya huko kwenye medula zao.

Wanapoagiza zifutwe wanamuagiza nani? Mtu anaekaa vikao vya sekretariet ndio anakuja kuwalalamikia watanzania. Sasa nadhani wanajuta mama aliporugusu mikutano ya kisiasa. Wamevurugwa.

Hizo kodi kandamizi zilianzishwa kwa manufaa ya nani? Aliyezipitisha ni nani? Anayetakiwa kuziondoa ni nani?
Kodi mmeanzisha nyie wenyewe,mnalalamika nyie kama ni kandamizi,mnaotakiwa kufuta ni nyie,halafu mnatoa maelekezo kwamba zifutwe. Mnataka raia ndio wazifute ?
Nyie mlikosea wenyewe kodi zenu na matozo yenu. Mkitaka futeni kimyakimya wala sio kuwafanya wananchi hamnazo
 
Back
Top Bottom