Waliochaguliwa ardhi university 2013/14

Jerhy

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
3,134
Reaction score
998
Tunayo pongezi kubwa kwa vijana wote waliochaguliwa kujiunga na chuo kikuu Ardhi kwa mwaka wa masomo 2013/14. Chuo kipo jijini Dar es Salaam karibu na UDSM.

Nianze kwa kukufahamisha jinsi ya kufika hapa, kwa wale watakaotoka mikoani , ukishuka tu ubungo kituo kikuu cha mabasi, toka nje uliza Sam Nujoma Road hii inanzia pale ubungo mataa kuelekea Mwenge hivo basi daladala za kwenda chuo zinapatikana pale darajani njia panda ya chuo kikuu, zimeandikwa Mwenge-Ubungo via Chuo kikuu nauli ni shilingi 400/= tu. Usikodi taksi 15,000/= hiyo utaijutia kwa sababu hapa hakuna atayekupokea ni wewe na begi lako kwani hata siku hiyo hutaonyeshwa mahali pa kulala hivo ni kuripoti na kusepa . Mpaka utakapo kamilisha malipo yote. Kwa hiyo Utashukia Ardhi au Geti dogo hapo utakuwa umefika Ardhi Univesity. jitahidi kuwahi kufanya usajili mapema ile wiki ya kwanza ili hatimaye ile wiki ya pili ndo majina ya accomodation hutolewa.

Mambo muhimu ya kuzingatia ni haya:
1. Chuo kina hostel ya waschana na wavulana yenye uwezo wa kubeba wanachuo 400 tu kila mwaka. Hivo ukiwahi kuripoti na kulipia pango basi ndo bahati yako pekee ambapo gharama zake ni120,000/= kwa semester per head. Ukikosa hosteli hiyo ipo nyingine nje ya chuo mitaa ya Lufungila ambayo gharama yake iko juu kidogo. Kwa hiyo njoo na fedha ya kutosha kuweza kujikimu.
2. Tuliowengi tumepanga mtaani survey na mlalakuwa huko vyumba ni kuanzia 60,000/= na kuendelea.
Hivyo basi jitahidini kuweka uhusiano mzuri kwenu wenye ndugu, jamaa na marafiki waliopo dar ili waweze kukuhifadhi kwa muda wakati ukisubiria mkopo loan bodi na kulipia pango.
3. Hakikisha unahudhuria orintation course kwa uaminifu zaidi kwani meng kuhusu mfumo mzima wa jinsi utakavyoishi hapo chuo hutolewa kwnye mhadhara huo, pia jitahidi kupsa ratiba ya matukio kutoka kwa mshauri wa wanafunzi.
4. Chuo hiki kinakazia zaidi elimu hivo wale wanaofikiria eti wiki ya kwanza hamna kitu sio kweli, ratiba inaheshimiwa zaidi kuliko wewe yaani profesa anaingia dakika tano kabla ya muda, anatoa logistic sheet ya kusaini mahudhurio baada ya dakika 15 kupita anaichukua kisha wale watakaofika kwa kuchelewa ni kwamba haeakuhudhuria lecture zake. Hawajali mpo 3 au 7 siku hiyo yeye atafundisha mada husika, na kutoa asgnment. Hivo mahudhurio yako mazuri ndo yatakuepusha na kurudia mitihani na diskondinuesheni.

5. Vifaa vya darasani katika fani za uchoraji vinapatikana katika stationary zetu chuo kwa bei nafuu zaidi.

Mwisho tunakukaribisha sana chuo kikuu Ardhi tarehe 14/10/2013​
 
asnt mkuu. sasa kwa 1st year,chuo knafnguliwa trh ngp? na orientation n ln? 2jpang kbs
 
tunashukuru mkuu kwa taarifa! Tutakutana kwenye SCHOOL OF CONSTRUCTION ECONOMICS AND MANAGEMENT(SCEM)
 
unaonekana umelewa weka hyo list ya waliochaguliwa,bado uko jkt
 
unaonekana umelewa weka hyo list ya waliochaguliwa,bado uko jkt

Vijana kuweni na subira taratibu za TCU ziko wazi kabisa kwamba baada ya kufanya selection awamu ya kwanza na ya pili basibmajina ya wote waliochaguliwa yalirejeshwa katika vyuo husika ili yakaguliwe kabla ya kuwekwa rasmi mtandaoni, hata hivyo baadhi ya vyuo husika vimeamua kujiridhisha na tayari yamewekwa katika website zao mfano: Jordan, Arch'Mihayo, Arusha univerty, Tumaini Makumira, etc. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za kiutendaji tarehe 25August2013, majina yalirudishwa tena TCU ambapo hapo sasa kikao cha pamoja kikaitishwa ili kuyajadili, na wskati hilo linaendelea ndipo nafasi nyingine ikatolewa kwa awamu ya tatu wanafunzi wale waliokosa kujisajili nao wanajaza sasa ikihusishwa wanachuo waliomaliza diploma NT6 Level, na matokeo yao kutoka rasmi mwezi July. Hivo basi tunayatarajia majina kutangazwa rasmi wiki hii au mwishoni mwa mwezi huu, kuhusu website ya TCU kutokufunguka ni kwamba database inapokuwa inawekwa faili zenye Gygabyte kubwa basi access yake inakuwa limited hivo kitumbua kiko jikoni jiandaeni na vikombe vya maziwa kujua chuo gani umepangwa, mie nisistize tu kuwa hakuna chuo cha kata Tanzania hao wanaosema hivo hawajui degree inatafutwaje.

Leo tarehe 28/08/2013 tutayaweka majina ya waliochaguliwa kuijunga na chuo kikuu Ardhi.

[ The Tanzania Commission for Universities (TCU) , has submitted to respective learning institutions names of candidates for verification before they are released by the end of this month.

TCU spokesperson, Mr Edward Mkaku, told The Citizen that the names would be verified by the councils of each learning institution before being sent back to the commission by the 25th of this month.

It was earlier reported that a total of 39,140 candidates had applied to join higher learning institutions in different programmes this year, but TCU confirmed that over 8,000 applicants will miss out. “After receiving the names... We will call a joint selection meeting,” he said.]
 
mbona hamna kitu ktk web yao....................?

The Tanzania Commission for Universities (TCU) , has submitted to respective learning institutions names of candidates for verification before they are released by the end of this month.

TCU spokesperson, Mr Edward Mkaku, told The Citizen that the names would be verified by the councils of each learning institution before being sent back to the commission by the 25th of this month.

It was earlier reported that a total of 39,140 candidates had applied to join higher learning institutions in different programmes this year, but TCU confirmed that over 8,000 applicants will miss out. “After receiving the names... We will call a joint selection meeting,” he said.
 
kwan wametoa majina ya waliochaguliwa kwenye web yao?

Chuo kikuu Ardhi kitafunguliwa rasmi tarehe 14/10/2013 wakati vijana wa supp wataanza tarehe 07/10/2013.

Hivi punde nitawawekea majina ya waliochaguliwa kujiunga na masomo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2013/14.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…