Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza 2023 hawa hapa

Waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza 2023 hawa hapa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wanafunzi 2,096 kati ya 2,194 waliofanya mtihani wa marudio wa darasa la saba, wamefaulu mtihani huo na kupangiwa shule za sekondari za serikali kuanza kidato cha kwanza.

Wanafunzi hao 2,194 wakiwemo wavulana 1,117 na wasichana 1,077 walifanya mitihani yao Desemba 21 na 22, 2022 kwa sababu ya matokeo yao kufutwa kutokana na udanganyifu.

“Jumla ya wanafunzi 2,180 wakiwemo wavulana 1,112 na wasichana 1,068 sawa na asilimia 99.36 walifanya mtihani wa marudio.

"Tamisemi imepokea matokeo hayo na wanafunzi 2,096 wakiwemo wavulana 1,073 na wasichana 1,023 sawa na asilimia 96.15 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wamepata sifa ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa shule za sekondari za Serikali,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ya Tamisemi inaeleza kwamba kwa kushirikiana na Kamati za Uchaguzi wa Waafunzi wa kidato cha kwanza katika mikoa husika, wamekamilisha mchakato wa kuwapangia shule wanafunzi wote waliofaulu.

Wanafunzi hao 2,096 wametakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa Jumatatu Januari 16.

Matokeo hayo yametoka ikiwa ni takribani wiki moja tangu wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023 kuanza masomo yao Januari 9, 2023.

BONYEZA Link hapa kuangalia https://www.tamisemi.go.tz/storage/...iwa Kidato cha Kwanza _Waliorudia Mtihani.pdf

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom