Waliofanikiwa zaidi maishani huamini vitu hivi vinne (4)

Peter Agostino

Senior Member
Joined
Sep 23, 2016
Posts
105
Reaction score
229
Mamilioni ya watu kote dunani tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu wamekuwa na ndoto kila mtu na za kwake. Wapo walioweza kuzitimiza ndoto zao na vilevile wengi walikufa na kuzikwa na ndoto zao kabla hawajafanikiwa kuzitimiza. Hii inamaanisha kwamba kama ndoto au malengo yangelikuwa ni vitu vya kushikika mfano wa magunia ya viazi, basi makaburi yangelijaa siku nyingi na duniani pengine pasingelikuwa tena na mahali pa kuzikia.

Mamilioni ya watu wenye ubunifu na vipawa vya aina mbalimbali wamekuwa wakiishi na ndoto zao wanazotamani kuzitimiza lakini kuna kitu kinachowavuta nyuma na kuwazuia kuzitimiza. Wana ndoto za kuanzisha biashara, kujenga nyumba, kununua kiwanja, kutunga kitabu, kupata mafunzo fulani, kuimba, kujifunza upishi, kwenda ulaya, kumiliki gari, kuoa, kuwa kiongozi wa siasa, kufanya hija maeneo matakatifu nk.

Lakini cha kushangaza ni kwamba wakati asilimia kubwa ya watu hao wakihagaika(wakistruggle) kutaka kutimiza ndoto zao hizo bila mafanikio, wapo baadhi ya watu (WALIOFANIKIWA) ambao wao huweza, tena kwa urahisi sana kutimiza malengo yao wanayojiwekea.

Kwa kweli kwa macho ya kawaida watu hawa huwa tunaona kama vile wamepata mafanikio kirahisi sana. Hivi ni kweli hupata mafanikio kirahisi namna hiyo? Na kama hivyo ndivyo basi wanatumia mbinu gani? Ni kitu gani kilichowapa nguvu wasikate tamaa na kuachana na biashara zao/malengo yao?

Katika makala hii ya leo nitakuelezea vitu vine 4 ambavyo watu wenye mafanikio makubwa huwa wanaviamini ili hali watu wa kawaida hufanya kinyume chake. Vitu hivyo ndivyo huwapa nguvu ya kutimiza malengo yao haraka na kwa urahisi, na zaidi ya hayo nitakueleza pia namna mtu anavyoweza akazitumia imani hizo 4 kufikia malengo yake ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakimkwepa.

Unapowafuatilia kwa undani utagundua kwamba, kile kilichowapa nguvu ni kile WALICHOKUWA WAKIKIAMINI, basi. Na kukosekana kwa kichocheo hiki kwa watu wa kawaida ndiko kunakosababisha makaburi au dunia kujaa mno ndoto na malengo yasiyotimizwa. Kile mtu anachoamini au kwa maneno mengine MTAZAMO WA AKILI(Mindset) ndiyo “petrol” au nishati inayochochea mafanikio kutokea, Wajasiriamali niliowataja na watu wote duniani walio na mafanikio makubwa, mafanikio yao hayo yalitokana na kile walichokiamini akilini mwao. Twende tukaone vitu hivyo sasa, Waliofanikiwa huamini;

1. Hakuna mafanikio ya ghafla,
Ni lazima uanze kidogokidogo ndipo baadae uweze kumalizia na kikubwa. Ingawa kweli wapo watu wanaochukua muda mfupi kuliko wengine kupata mafanikio, lakini kwa ujumla mafanikio yeyote yale makubwa ni matokeo ya mchakato wa muda mrefu.

Hatari ya kuamini katika mafanikio ya haraka ni kwamba utakata tamaa mara tu utakapokutana na kikwazo hata ikiwa ni kidogo, hii tena ni sababu nyingine ya dunia kujaa ndoto nyingi zisizotimia kwani watu wengi hujaribu mara moja, na wanapoanguka, huacha mara moja wakiamini wazo lao halikuwa sahihi.

2. Ukikosea mara ya kwanza hujashindwa bado kwani siyo jaribio lako la mwisho.
Kuna mfano mmoja maarufu wa mgunduzi wa taa hizi za umeme tunazotumia mpaka leo hii (balbu) kufeli karibu mara 9999 na mara ya elfu 10 ndipo akaja kufaulu. Angeachilia pale pale mara ya kwanza tu alipofeli, leo hii pengine dunia ingelikuwa bado inatumia vibatari na taa za mafuta ya wanyama kama zama hizo.

Mbaya zaidi katika imani hii namba 2 ni pale mtu unapokosea na kisha watu wengine kukubeza; “Hee! Ulishindwa kiangazi masika utaweza?”, “Umeshindwa na taa ya Mungu mchana, utaweza na taa ya Mzungu usiku?” nk. hayo ni baadhi tu ya maneno watu hutumia kuzidi kuwavuja moyo wenzao wanaoshindwa jambo.

Na wewe ukiwa na mtazamo potofu(negative mindset) utakata tamaa kweli na kujiona hufai, huwezi na wala hutokaa uweze tena kitu maisha yako yote.

Lakini wewe badala ya kuvunjika moyo, hebu jaribu kutofautisha utendaji wako na uwezo mkubwa uliojificha ndani yako ambao kama utaamua kuutumia kila mtu anaweza akashangaa. Jiulize tena, ni nani aliyezaliwa akiwa anajua kusema, kuandika au kuhesabu? Vyote tulikuja kujifunza siyo?

Aliye na mtazamo sahihi wa akili huamini kuwa, duniani hakuna aliyezaliwa akiwa anafahamu kitu, kila taaluma duniani inaweza kufundishika na mtu yeyote yule ana uwezo wa kujifunza taratibu mpaka akawa bingwa kabisa katika fani yeyote ile. Uwezo wa akili ya binadamu yeyote yule ni wa ajabu sana kiasi kwamba hakuna asiloweza kujifunza akaelewa.

3. Ili ufanikiwe fanya kile unachokipenda.
Huwezi kufanikiwa katika shughuli usiyoipenda na usiweke malengo yako kwenye pesa kwanza bali fanya kwa uaminifu kile kitu unachokipenda zaidi kiasi kwamba watu macho yao yote yakutazame wewe. Watu wa kawaida hudhani kimakosa kwamba wanaofanikiwa hufanya kwa kujilazimisha vitu au kazi wasizozipenda mpaka wanafanikiwa, kumbe ukweli siyo hivyo kabisa. Huwezi kufanikiwa kwa kufanya kitu usichokipenda.

4. Mafanikio siyo kupaa tu, kuna kuanguka pia.
Kwa mfano kwenye Ujasiriamali tunajifunza kwamba, tunapochukua hatari katika biashara kuna mambo mawili, kupata faida au kupata hasara, na vyote viwili kila kimoja kina nafasi sawa ya kutokea. Hii inamaana kwamba unapopanga kufanikiwa vilevile panga na kuanguka. Mara nyingi watu wanaoanguka na kuinuka wakaendelea na safari ndio ambao huja kuibuka washindi mwishoni.
 
Ila ufanikiwe inabidi uwe Freemason
 
Naongezea...

5. Mafanikio hayapo up to you pekee.
Mafanikio yanatokea pale your skills intersects with opportunity; na opportunity hutengenezwa na external circumstances pamoja na a little bit of you.
Hii inamaanisha kupata kimojawapo such as labda skills pekee au fursa pekee, hakitafanyika kitu.

References:
Tazama watu wengi waliofanikiwa. Fuatilia taratibu historia zao katika kila step. Wengi wanadhani wanajua siri ya mchezo, lakini ukiingia deep, utaona tu ni kwamba ni coincidence/luck ya pale uwezo wao ulipokutana na fursa.
 

Hahaha
Kwa kiswa English umeua
Duuuh we noma
 
Poooòiiooooo
............ Msasani....
ooooo9ooooooooooooooiooio oookllllllooooooloooooooo9oooooœoooooooooooooooooo ofooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo you9oo9ooooøooo9ooooooooooo9oooooooooooooooooooooooo ook*ooloooooooooooooo[emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193][emoji193]
 
Safi sana, mkuu.
 
Mimi nilichojifunza watu wanaofanikiwa ni wale wanaofight sana kupata passive income kuliko pato lile la kila siku
 
It's good article.[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…