Walioichambua Almasi Sana Mwisho Waliambulia Mkaa!!

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
291
Reaction score
198
Mwenye kutaka rafiki asiye kuwa na Dosari, basi ataishi mpweke daima.

Mwenye kutaka Mke au Mume ambaye hana mapungufu, ataishi bila ya kuoa au kuolewa (Bachelor) mpaka siku ya kufa kwake.

Mwenye kutaka ndugu asiye kuwa na matatizo, ataishi akimtafuta milele.

Mwenye kutaka mtu wa karibu aliyekamilika, daima ataishi akiukata udugu.

Tuvumilie matatizo ya wenzetu pamoja na changamoto zao, ili turejeshe hali ya maelewano kati yetu.

Unapotaka kuishi kwa furaha maishani, basi usitafsiri kila kitu unachokiona au kukisikia.

Wala usichunguze sana kila kitu kilichopo mbele yako.

Wala usichambue kila kitu unachokiona au kukisoma.

Hakika ya wale walioichambua Almasi sana, mwisho wa siku waliikuta ni Mkaa.

Usiwahukumu watu kutokana na mandhari (muonekano wa nje), vyo vyote vile walivyo.

Fahamu ya kuwa pamoja na yote hayo, bado ni wanadamu kama wewe (uhalisia wao).

[HASHTAG]#Tuvumiliane[/HASHTAG] hakuna mkamilifu isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee !!!.
 
Uvumilivu ni muhimu lakini kuna Kiasi katika Uvumilivu.

Nilitegemea WCB kwa ninavyowapenda wawe na uvumilivu kwa Imani Ya Kikristu lakini inaonekana sivyo. Wenye makali wanawakandamiza kinamna wenye ncha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…