Wana jamnvi leo nimeshangaa sana na kusikitika kusikia wapo form 4 ambao walikuwa na div 4 na walijiunga na vyuo vya ualimu, kwa sasa wanafunzi hao waliachishwa kusoma na kuambiwa warudie hadi wapate div 3 ndio wataruhusiwa kuendelea au kusomea ualimu, nauliza kwanini wasingewaacha halafu wanaojiunga wapya ndio wapewe masharti hayo, maana hata mtu akifanya mtihani na asipate div 3 imetoka, amelipa ada na amepoteza muda mwingi kusoma inakuwaje. lazima tuwe wangwana sisi sote ni watanzania, Jakaya Kikwete aliporuhusu hili lilikuwa jema kwa wengi na walimshukuru Mola, sasa tuangalie tunafanya nini kuzalisha form 3 ili wajiunge na vyuo vya ualimu haijasaidia bado kuziba getu ya uhaba wa waalimu wala kuwafanya wawe na performance ya juu wapo watakao kuwa nayo na wengine ndo hivyo cha msingi ni kuwa upgrades na kuwajengea uwezo zaidi katika fani hiyo.