Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, ambaye alihoji "
Katiba mpya ya nini?" kwa mujibu wa cheo chake kama mshauri mkuu wa masuala ya sheria wa serikali lazima awe mjumbe wa Constitutional Review Commission ambayo Rais Kikwete anatarajia kuiunda.
Tunapaswa kujiuliza Watanzania wanahitaji nini? Mimi binafsi ukiweka wadhifa wangu kando, bado sioni haja ya Katiba mpya, lakini kama ni Watanzania wanataka mpya sawa, wakitaka marekebisho pia sawa, Werema alikaririwa akisema na gazeti la serikali, Habari Leo.
Kila mtu anazungumza kama bata, watu wanazungumza kibatabata, lazima tujiulize Watanzania wanataka nini? Wakati fulani iliwekwa vifungu vya haki za binadamu kuanzia kifungu cha 12 hadi 29 kwa kuwa vilihitajika, tuzungumze si kutishana, alisisitiza Jaji Werema huku akitolea mfano Katiba ya India ya mwaka 1948 iliyofanyiwa marekebisho mara 50.
Sasa kwa msimamo wake huu, sidhani kama mchango wa AG kwenye tume ya kupitia katiba kama utakuwa na tija.
Huko kwa jirani zetu kenya, wao waliunda Committee of Experts kuandaa katiba mpya. Bofya hapa ili kupata taarifa za uzoefu wa Kenya kwenye katiba mpya:
About us
Wajumbe wa kamati hiyo ya Kenya ya kupitia katiba walikuwa hawa hapa:
Profiles of members of the Committee of Experts
Nimevutiwa na kauli mbiu yao --
Katiba mpya ni SASA kama siyo SASA ni SASA HIVI!.
Katiba Mpya, Tanzania Moja...