Waliomteka mfanyabiashara, kuomba rushwa wakiri mashtaka

Waliomteka mfanyabiashara, kuomba rushwa wakiri mashtaka

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
753
Reaction score
1,812
Askari polisi watatu pamoja na raia sita akiwemo mfanyabiashara maarufu wa Madini a Tanzanite, Lucas Mdeme wanaotuhumiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi wamekiri makosa kwa kuandika barua kwa DPP.

Wameandika barua ya kukiri mashataka sita wanaokabiliwa nayo ikiwemo uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia fedha ya awali shilingi milioni 10 kati ya milioni 30 walizohitaji kutoka kwa Sammy Mollel

Watuhumiwa hao ambao walifikishwa mahakama hapo mapema leo kabla ya kuahirishwa, wakili wa utetezi Charles Kagirwa mara baada ya hakimu wa kesi hiyo kusema upelelezi wa kesi hiyo unaendelea ndipo wakili huyo alisema kuwa wateja wake tayari wameaandika barua ya kukiri mashtaka hayo.

Hata hivyo waendesha mashtaka wa serikali Adelaide Kassalay na Agnes Hyera walimweleza Hakimu Ngoka kuwa wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo kwani upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Hakimu mkazi mfawidhi wa Arusha,Rose Ngoka amesema kuwa kesi hiyo namba 3/2021 imeahirishwa hadi February 24 mwaka huu kwaajili ya kutajwa hivyo watuhumiwa wataendelea kukaa rumande katika gereza la kisongo kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana .

Januari Saba Mwaka huu Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu kushikiliwa kwa Askari polisi Watatu na Raia Sita kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ya Germs and Rocks Ventures iliyopo Jijini humo.

Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na tukio hilo ni Askari Polisi Intelijensia Mkoa wa kinondoni mwenye namba G.5134 DC Heavenlight Mushi,Askari Polisi Intelijensia Makao Makuu H.125 DC Gasper Paul na Askari Polisi Kazi za kawaida Mkoa wa Dodoma H.1021 PC Bryton Murumbe ambao wamefukuzwa kazi ndani ya Jeshi hilo.
 
Screenshot_20210210-164715.png

Waliokuwa askari wa Jeshi la Polisi na wenzao watano wanaokabiliwa na mashtaka ya kumteka mfanyabiashara wa madini, Sammy Mollel na kumuomba rushwa ya Sh30 milioni wameandika barua za kukiri mashtaka sita.

Mashtaka waliyokiri ni ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia fedha kinyume na utaratibu ambapo awali walishachukua Sh10 milioni kati ya milioni 30 walizohitaji kutoka kwa Mollel.

Wakili upande wa utetezi Charles Kagirwa amesema wateja wake wameshaandika barua ya kukiri mashtaka hayo.

Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2021 leo Jumatano Februari 20,2021 imesikiliwa na hakimu mkazi mfawidhi, Rose Ngoka ambaye alisema hajaridhishwa na barua yao ya kukiri mashtaka sita na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2021 itakapotajwa tena.

Kabla ya kupandishwa kizimbani, askari hao walishtakiwa kijeshi na walibainika na tuhuma na kufukuzwa kazi kwa kosa la kupokea rushwa ambao ni Heavenlight Mushi aliyekuwa kitengo cha Intelijensia Mkoa wa kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, Gasper Paul kitengo cha Intelijensia makao makuu Dodoma na Bryton Murumbe.

Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Joseph Chacha, Leonila Joseph, Nelson Lyimo na Omary Alphonce.
Washtakiwa wote wamerudishwa katika gereza la Kisongo kwa kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.
 
Kuna mengi sana ya kufikirisha. Kwani hawa askari shida ni nini hadi wafanye yote hayo?🤔
 
Kuna mengi sana ya kufikirisha. Kwan hawa askari shida ni nini hadi wafanye yote hayo?[emoji848]
Tamaa tu ya kutaka kuishi maisha mazuri. Ku drive gari kali, kujenga mjengo wa heshima, nk. Nothing more.
 
Kuna mengi sana ya kufikirisha. Kwani hawa askari shida ni nini hadi wafanye yote hayo?[emoji848]
Na wao wanataka kumiliki Subaru hapo Chuga ili waopoe pisi kali kitaa mkuu.... [emoji23] [emoji23]
 
adelaide kassala my dear kaza buti, huwa nakusoma sana hata kwenye ile kesi ya mkami. sijui umeifikisha wapi.
Mungu akulinde na wabaya.
 
Back
Top Bottom