Waliomuibia mchumba wa Dk Slaa mbaroni

Waliomuibia mchumba wa Dk Slaa mbaroni

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Waliomuibia mchumba wa Dk Slaa mbaroni
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Friday, 29 July 2011 22:28 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Aziza Masoud na Shakila Nyerere
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, inawashikilia watu wanane wakiwamo waliomvamia mke wa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, Josephine.Josephine alivamiwa na majambazi hao na kumpora vitu mbalimbali Julai 13, mwaka huu saa 11.00 jioni eneo la Mwenge jirani na Suma JKT, akiwa na gari aina ya Harrier.
Katika tukio hilo majambazi hao walifyatua risasi kabla ya kuvunja kioo cha gari hilo kwa nyundo, kisha kumwibia mkoba uliokuwa na vitu mbalimbali.Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema kufuatia tukio hilo, wamekamata majambazi watano ambao walihusika na uvamizi.Pia, polisi imeahidi kutoa Sh3 milioni kwa mtu atayefanikisha kukamatwa kwa jambazi sugu anayetambulika (jina tunalo).
Kova alisema kutokana na jambazi huyo kutafutwa kwa muda mrefu, sasa wameamua kutoa zawadi kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye anaongoza kundi la majambazi hatari.Alisema mtuhumiwa huyo wenye muonekano wa utanashati anapatikana maeneo ya Kinondoni kwenye mikusanyiko ya vijana.
Katika hatua nyingine, polisi inawashikilia madereva watano kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa askari wa usalama barabarani maeneo tofauti.Watu hao walikamatwa baada ya kuwashawishi askari wa usalama barabarani kuchukua rushwa baada ya kufanya makosa ya uvunjaji sheria za barabarani na kwamba, upelelezi unaendelea ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Wakati huohuo, mwanaume asiyefahamika alifika kituo cha polisi akiwa na bahasha yenye nembo ya Benki ya NMB, yenye bastola na kumkabidhi ofisa wa polisi aliyekuwapo kisha kutoweka.
Kwa mujibu wa Kova, mtu huyo alifika kituoni hapo na kumkabidhi bahasha hiyo askari, huku akimwambia achukue mzigo wake ambao alitumwa kumletea na baada ya hapo alitoweka, baada ya kufungua bahasha hiyo alikuta bastola aina ya Browing Court yenye namba A71 iliyokuwa na magazine yenye risasi 13.
Alisema huenda mtu huyo ameamua kujisalimisha kufuatia agizo la Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, kuwataka watu kusalimisha silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[h=4]Comments [/h]


-1 #1 Mfikiri Mbali 2011-07-30 01:53 Mchumba???? kweni wazee wana wachumba pia?? na je huu ni utamaduni wetu?? mafundisho gani tunapata kutoka kwa kiongozi anayepigiwa debe urais?? Tafakari. Nakemea sana kitendo cha wizi.
Quote







Refresh comments list
 
huu ni wizi wa kawaida tu usihusishwe na siasa...................
 
Rutashubanyuma;2293420] #1 Mfikiri Mbali 2011-07-30 01:53 Mchumba???? kweni wazee wana wachumba pia?? na je huu ni utamaduni wetu?? mafundisho gani tunapata kutoka kwa kiongozi anayepigiwa debe urais?? Tafakari Nakemea sana kitendo cha wizi
Kwa vile kichwa cha habari na habari nzima ni wizi na ujambazi alau ungeanza kukemea ningekuelewa lol.
Nikuulize kwani uchumba maana yake ni nini? Na uzee unaanzia na kuishia wapi? Kuna watu wanaoa wakiwa na zaidi ya 60 je kuna maadili wamekiuka? Utamaduni wa mtanzania katika mambo ya ndoa ni upi? Je mahusiano ya ndoa ya rais au mgombea yanatakiwa yawaje?
 
Jamani naomba asiitwe mchumba, uyu our president alochakachuliwa kaishi na uyu mama zaidi ya mwaka sasa, uyu ni mkewe kabisa, plz asishushiwe hadhi
 
Back
Top Bottom