Katika kuficha ukweli kuhusu aliyofanyiwa, jumuiya hiyo kwa muda wa karne nzima imekuwa ikidai eti alikuwa mfanyakazi wa bustani hiyo na wakati mwingine kujichanganya katika maelezo yake.
Mwaka 1916, kufuatia kifo cha Ota Benga, habari iliyoandikwa na gazeti la New York Times ilitupilia mbali madai ya mwafrika huyo kuwa mfanyakazi wa bustani hiyo na kueleza kwamba mwanadamu huyo alikuwa anashikiliwa katika bustani hiyo akiwa mmoja wapo ‘wanyama’ wa maonesho katika kizimba alichokuwa akiishi na nyani na tumbili.
Hatua hiyo, ilipingana na taarifa nyingi katika magazeti ambazo kwa muongo mmoja zilijaribu kufunika kuhusu kudhalilishwa kwa mwafrika huyo.
New York Times pekee, baada ya kufaya uchunguzi wa kina lilichapisha makala kadhaa juu ya madhila aliyopitia Mkongomani huyo ikiwemo habari iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho. "Mtu pori aishi kwenye kizimba na nyani katika Bustani ya Bronx Park Apes".
Mwaka 1974, William Bridges, ofisa habari wa bustani hiyo aliibuka na kudai kwamba kilichotokea hasa kuhusu mwafirika huyo hakijulikani vyema hata kwa wao.
Katika kitabu chake, Ukusanyaji wa Wanyama, Bridges aliuliza: "Je, Ota Benga alichukuliwa ili kufanywa maonesho mithili ya mnyama wa ajabu na adimu?" Swali hili anaweza kulijibu mtu aliyekuwa anatunza kumbukumbu za bustani (ambaye alishafariki dunia).
"Kwamba alifungiwa kwenye kizimba cha nondo ili watu wanaokuja kwenye maonesho wamtazame inaonekana si kweli," aliendelea kuandika akipuuza ushahidi katika nyaraka kadhaa na picha zilizoonesha kwamba Mwafrika huyo alilinganishwa na mnyamapori.
Bridges alizidi kudai kwamba anachoona Ota Benga alikuwa akivutiwa kuishi New York na kufanya kazi kwenye bustani hiyo ya Wanyama.
Urafiki kati ya watekaji na mateka?
Mwaka 1992 kilichapishwa kitabu kingine kilichoandikwa na mjukuu wa Samuel Verner, mtu ambaye alikwenda Kongo akiwa na silaha kumteka nyara Ota Benga na wengineo kadhaa ili kuja kuwafanya maonesho makubwa ya kimataifa ya mwaka 1904.
Kitabu hicho kilidai kwamba Verner aliunga urafiki na Ota Benga na kuamua kuja naye New York kwa mapenzi yake.
Kuna gazeti moja baada ya uchapishwaji wa kitabu hicho cha mjukuu wa Verner pia lilidai kwamba Ota Benga alifurahia kuja New York wakati ukweli ni kwamba alikamatwa kwa mtutu wa bunduki na alipinga vikali kutenganishwa na jamii yake.
Kwa hivyo kwa zaidi ya karne moja, watu wa taasisi iliyomnyanyasa vibaya Ota Benga, na kizazi chao, walificha rekodi sahihi za kihistoria kwa kuja na simulizi zisizo za kweli katika kuuhadaa ulimwengu.
Hata sasa, ingawa Samper ameomba msamaha kwa hatua ya Bustani yao kumuonyesha Ota Benga kama ‘mnyama mwitu’ kwa "siku kadhaa" bado kuna ukakasi kwani ukweli ni kwamba alizuiliwa kwa majuma matatu baada ya kukamatwa mateka na kutupwa kwenye kizimba akiishi na nyani na tumbili.
Kwa sasa bustani hiyo imeweka nyaraka kwenye mtandao kuhusu kilichojiri kwa Ota Benga alipokuwa anashikiliwa bila ridhaa yake kwenye bustani hiyo.
Nyaraka hizo tayari zimetajwa katika kitabu cha Miwani: Maisha ya kushangaza ya Ota Benga, kilichochapishwa 2015.
Ndani ya miaka mitano tangu kuchapishwa kwa kitabu changu hicho, maofisa wa bustani hiyo walikuwa wamegoma kukiri ukweli na kuomba radhi na pia walikuwa hawataki kujibu maswali ya wanahabari.
Na wakati huo nilipotembelea nyumba ambamo Ota Benga alikuwa akishikiliwa huku akiwa amevaa mavazi ambayo yalikuwa hayawezi kumkinga vyema na baridi, lakini sasa kimefungwa dhidi ya umma unaokwenda bustanini hapo.
Chumba bora katika nyumba ya nyani
Sasa Samper anasema: "Tunajuta kwamba watu na vizazi vingi vimeumizwa na kitendo hiki na pia kwa kushindwa kwetu tangu awali kulaani yalitotokea.”
Samper pia anajaribu kuonesha kwamba katika nyumba ya manyani, Ota Benga alikuwa na chumba kizuri, jambo ambalo pia linaacha mashaka.
Ni vyema Jumuiya hiyo ikaendelea kukiri ukatili uliofanyika na kupokea ushauri wa kuanzisha kituo cha elimu dhidi ya ubaguzi wa rangi kitakachoitwa kwa jina Ota Benga.
Ota Benga alikuwa nani?
Mwafrika huyu ambaye alikuwa mfupi (mbilikimo) alitekwa nyara Machi 1904 na mfanyabiashara wa Marekani Samuel Verner kutoka iliyokuwa ikiitwa wakati huo Belgium Congo.
Umri wake wakati anatekwa haufahamiki vyema lakini inadhaniwa alikuwa mtoto wa miaka 12 au 13
Alisafirishwa kwa meli na kisha, akiwa na wezake wanane walipangwa kwa ajili ya maonesho.
Maonesho hayo yalifanyika katika kipindi cha majira ya baridi huku waafrika hao wakiwa na nguo ambazo zilikuwa haziwakingi vyema na baridi.
Shukrani kwa BBC na HabariLeo.