Walioongoza kidato cha nne 2007 watajwa

Walioongoza kidato cha nne 2007 watajwa

Mswahili Old Acc

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2006
Posts
488
Reaction score
24
Walioongoza kidato cha nne watajwa

*Watatu wanatoka Mtakatifu Francis Mbeya
*Wakabidhiwa zawadi zao na Rais Kikwete

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imewatangaza wanafunzi 12 bora waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, huku msichana Evelyne Lupimo, kutoka Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Francis, Mbeya, akishika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa Sh800,000.

Akitangaza wanafunzi hao Ikulu jana, ambako walikwenda kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete wakiambatana na wazazi na walimu wao, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margareth Sitta, alisema wanafunzi hao walipata alama za juu kuliko wengine.

Sitta alisema wanafunzi hao wako kwenye makundi manne; wanafunzi watatu wasichana waliofanya vizuri zaidi kutoka shule za serikali na wengine watatu kutoka shule zisizo za serikali. Pia wapo wanafunzi watatu wavulana kutoka shule za serikali na watatu kutoka sekondari zisizo za serikali.

Wasichana watatu waliofanya vizuri zaidi kutoka sekondari zisizo za serikali ambao wote wametoka Sekondari ya Mtakatifu Francis, Mbeya, ni Lupimo, Erika Kafwimi na Ines Muganyizi.

Wavulana kutoka kundi hilo ni Invokafti Munisi (Agape); Abraham Mgowano (Loyola) na Claverfred Mhidze (Mtakatifu Joseph Kilocha).

Wasichana kutoka sekondari za serikali ni Sarah Wangilisasi (Kilakala), Naomi Elibariki (Jangwani) na Hellena Mnegena (Msalato). Wavulana waliofanya vizuri kutoka sekondari za serikali ni Shaaban Yusuph (Tanga), Mwasapi Kihongosi (Kibaha) na Mandela Makalala (Arusha).

"Ufaulu wa wanafunzi hawa ni wa kujivunia wenyewe, familia zao, shule zao na taifa kwa jumla. Wamefanikiwa kupata alama za juu zaidi katika masomo yao yote. Tunaamini matokeo haya mazuri yametokana na juhudi yao kubwa katika masomo, kazi nzuri ya walimu na msaada waliopata kutoka kwa wazazi wao," alisema Sitta.

Kutokana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuthamini ufaulu wa wanafunzi hao, licha ya kutunukiwa vyeti na Rais Kikwete, pia walizawadiwa Sh300,000 kila mmoja na vitabu vya masomo ya vidato vya tano na sita vya Sh200,000 kila mmoja.

"Mwanafunzi Evelyne Lupimo ambaye amefanya vizuri zaidi kupita wote ataongezewa Sh500,000 kwa kushika nafasi hiyo," alisema Sitta na kuongeza kuwa, sherehe hiyo itakuwa chachu kwa wanafunzi wote kuongeza juhudi katika masomo.

Tukio la Rais Kikwete kuwafanyia sherehe wanafunzi bora ni la kwanza la aina hiyo na Waziri Sitta alisema hatua hiyo imeonyesha jinsi Rais Kikwete anavyothamini maendeleo ya elimu nchini na ishara ya mhimili wa kutegemewa katika suala hilo.

Serikali imekuwa ikichukua hatua za kuhamasisha wanafunzi kufaulu vizuri na wanafunzi waliofaulu vizuri darasa la saba kwenda kidato cha kwanza mwaka jana, walipelekwa bungeni Dodoma kwa ajili ya kukutana na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Spika wa Bunge, Samwel Sitta na wabunge.
 
Walioongoza kidato cha nne watajwa

KikweteShein_frontpic_24.jpg

President Kikwete with Evelyine Lupimo who emerged as the Best student in the country in her O'Level exams among the 12 students who were awarded for performing well in various categories.​

normal_Jakaya_Kikwete_2_126~0.jpg

President Jakaya Mrisho Kikwete this morning awarded 12 students who emerged top performers in their O'Level Exams last year.The Brief but colourful ceremony was held at State house Dar es salaam.​

*Watatu wanatoka Mtakatifu Francis Mbeya
*Wakabidhiwa zawadi zao na Rais Kikwete

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imewatangaza wanafunzi 12 bora waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, huku msichana Evelyne Lupimo, kutoka Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Francis, Mbeya, akishika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa Sh800,000.

Akitangaza wanafunzi hao Ikulu jana, ambako walikwenda kupongezwa na Rais Jakaya Kikwete wakiambatana na wazazi na walimu wao, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margareth Sitta, alisema wanafunzi hao walipata alama za juu kuliko wengine.

Sitta alisema wanafunzi hao wako kwenye makundi manne; wanafunzi watatu wasichana waliofanya vizuri zaidi kutoka shule za serikali na wengine watatu kutoka shule zisizo za serikali. Pia wapo wanafunzi watatu wavulana kutoka shule za serikali na watatu kutoka sekondari zisizo za serikali.

Wasichana watatu waliofanya vizuri zaidi kutoka sekondari zisizo za serikali ambao wote wametoka Sekondari ya Mtakatifu Francis, Mbeya, ni Lupimo, Erika Kafwimi na Ines Muganyizi.

Wavulana kutoka kundi hilo ni Invokafti Munisi (Agape); Abraham Mgowano (Loyola) na Claverfred Mhidze (Mtakatifu Joseph Kilocha).

Wasichana kutoka sekondari za serikali ni Sarah Wangilisasi (Kilakala), Naomi Elibariki (Jangwani) na Hellena Mnegena (Msalato). Wavulana waliofanya vizuri kutoka sekondari za serikali ni Shaaban Yusuph (Tanga), Mwasapi Kihongosi (Kibaha) na Mandela Makalala (Arusha).

"Ufaulu wa wanafunzi hawa ni wa kujivunia wenyewe, familia zao, shule zao na taifa kwa jumla. Wamefanikiwa kupata alama za juu zaidi katika masomo yao yote. Tunaamini matokeo haya mazuri yametokana na juhudi yao kubwa katika masomo, kazi nzuri ya walimu na msaada waliopata kutoka kwa wazazi wao," alisema Sitta.

Kutokana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuthamini ufaulu wa wanafunzi hao, licha ya kutunukiwa vyeti na Rais Kikwete, pia walizawadiwa Sh300,000 kila mmoja na vitabu vya masomo ya vidato vya tano na sita vya Sh200,000 kila mmoja.

"Mwanafunzi Evelyne Lupimo ambaye amefanya vizuri zaidi kupita wote ataongezewa Sh500,000 kwa kushika nafasi hiyo," alisema Sitta na kuongeza kuwa, sherehe hiyo itakuwa chachu kwa wanafunzi wote kuongeza juhudi katika masomo.

Tukio la Rais Kikwete kuwafanyia sherehe wanafunzi bora ni la kwanza la aina hiyo na Waziri Sitta alisema hatua hiyo imeonyesha jinsi Rais Kikwete anavyothamini maendeleo ya elimu nchini na ishara ya mhimili wa kutegemewa katika suala hilo.

Serikali imekuwa ikichukua hatua za kuhamasisha wanafunzi kufaulu vizuri na wanafunzi waliofaulu vizuri darasa la saba kwenda kidato cha kwanza mwaka jana, walipelekwa bungeni Dodoma kwa ajili ya kukutana na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Spika wa Bunge, Samwel Sitta na wabunge.

I like this ......
Uongozi wa nchi unaonyesha jinsi unavyothamini Elimu, pia hawa wanaangaliwa na wenzao kama role models.

Those saying our education is in shambles, to them I say we are coming fast, soon we will be breathing on their necks!!..
 
Habari za kuaminika hakuna hata mmoja wa wale uliouliza. (Joke)
 
kama hakuna mchagga, mhaya, au mnyakyusa basi nitakubali kuwa Tanzania elimu inaendelea kuwafikia watu wengi.. anyway... kwanini shule inayoongoza inatoka Mbeya tena...mweh.. huu ukabila sasa umezidi hata watu kufaulu waende kufaulu kwenye moja wapo ya mikoa "ile ile"....
 
Kwenye hiyo orodha kuna mchanganyiko wa makabilka wakiwemo hao uliowataja.Pili Hata hao waliofauli kwenye hizo shule kwenye hiyo mikoa zilizomo hizo shule si wenyeji wa mikoa hiyo.
 
Back
Top Bottom