Uchaguzi 2020 Walioongoza kura za maoni Hai Kilimanjaro watangazwa rasmi kuwa wamepitishwa na CCM kugombea Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Walioongoza kura za maoni Hai Kilimanjaro watangazwa rasmi kuwa wamepitishwa na CCM kugombea Oktoba 2020

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza.

Katibu wa CCM wilaya yaHai mkoani Kilimanjaro, siku ya leo baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa udiwani kupitia viti maalumu, amewatangaza rasmi madiwani wa kata,viti maalum na mbunge Saashisha kuwa wamepitishwa rasmi kugombea nafasi zao walioongoza kwenye kura za maoni bila matatizo. Katika tukio la leo Saashisha alikuwa mgeni rasmi na ameshatambulishwa kuwa ndiye mbunge wa CCM Hai.

Kwa mantiki hiyo tunamshangaa Kwanini majimbo mengine makatibu wa CCM wilaya hawatangazi wagombea waliopata Kura nyingi za maoni kuwa wamepitishwa? Au Kuna agenda ya kukata majina ya walioshinda Kura za maoni?

Msimamo wa katibu wa CCM wilaya ya Hai unaonyesha hakuna haha ya vikao vya juu kupitia majina ya Kura za maoni. Msipomfuatilia huyu.

Katibu wa CCM wilaya ya Hai kwa kauli na maamuzi yake yajayo yatafurahisha. Usiku mwema.
 
Kwahiyo anaenda kinyume na utaratibu wao kama Polepole alivyo tangaza.
 
Kwahiyo anaenda kinyume na utaratibu wao kama Polepole alivyo tangaza.

Ongeza sauti. Katibu wa CCM wilaya ya Hai hajui Kuna wakubwa zake ndani ya chama tawala, anafanya anavyotaka, anajibu anavyotaka, anatekeleza anavyotaka na hatambui uwepo wa DC wa wilaya ya Hai, hata kidogo.ninashauri viongozi wa CCM mkoa na Taifa, pitieni vizuri mienendo ya huyu katibu haswa kwenye uchaguzi huu.

Ikiwezekana line yake ifukuliwe utaisikia maajabu aliyokuwa anawadiliana nayo kuhusu mambo ya fedha, ana changamoto nyingi japo anakidanganya chama kuwa atakomboa Jimbo la Hai, jimbo wananchi wenyewe wameshalikomboa bali yeye ataliangusha akicheza, asipofuatiliwa mapema.
 
Back
Top Bottom