#COVID19 Waliopatiwa chanjo waombwa kutoa ushirikiano wanapotakiwa kufanyiwa tafiti

#COVID19 Waliopatiwa chanjo waombwa kutoa ushirikiano wanapotakiwa kufanyiwa tafiti

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali imeanza mchakato wa utafiti wa kuwapima afya baadhi ya watu waliopata chanjo ya kuzuia Uviko-19 ili kujua maendeleo ya afya zao.

Lengo la utafiti huo ni kubaini mwenendo wa afya za waliochanjwa ili kuona wastani wa kinga zao na namna wanavyoweza kujikinga.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Oktoba 27, 2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi wakati akitoa taarifa kuhusu hatua za utekelezaji wa miradi ya afya kwa maendeleo.

Utafiti huo utafanyika kwa kutumia sehemu ya Sh1.3 trilioni ambazo zilitolewa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) kwa ajili ya mapambano ya Uviko-19.

Katibu Mkuu amesema katika utafiti huo watapata ukweli wa maendeleo kwa waliopata chanjo wastani wao katika maendeleo ya afya na kama kunahitajika kujikinga zaidi.

Amewataka Watanzania kutokuwa na hofu katika utafiti huo kwani hauna nia mbaya zaidi ni maboresho juu ya kinga na yatakwenda kuwa msaada zaidi kwa wananchi.

"Tunaweza kukuta mfano mtu ana kinga kwa asilimia 70 au 80, hivyo sisi tutajua sasa mtu huyo tumsaidiaje ili kufikia asilimia 100 ya kinga yake, watu wasihofu hata kidogo," amesema Profesa Makubi.

Kauli ya Katibu imekuja huku Serikali ikitangaza kuwa chanjo ya awamu ya kwanza ya Johnson & Johnson zaidi ya dozi milioni moja zimekwisha na sasa Watanzania wanachanja aina ya Sinopharm ambayo imetoka nchini China.

Chanzo: MWANANCHI
 
Aiseeee! Yaan Watanzania wamekua sehemu ya majaribio! Chanjo ya USA hawajakaa sawa inakuja ya CHINA wakimaliza inakuja ya FRANCE, lol

Inatishaaaa!
 
Halafu ripoti iende kwa waamerika na wachina kuwa dawa zao ni nzuri
 
Anzeni na huyu

0FCDC30B-6E75-4424-ACE3-E2561F65137B.jpeg
 
Back
Top Bottom