Kuna kata moja wilaya ya Temeke idadi iko hivi (kwa mujibu wa matokeo ya udiwani yaliyobadikwa)
Waliojiandikisha kupga kura katika Kata hiyo ni 12,393
Walipiga kura ni 4,815 (asilimia 39)
kunaweza kuwa na maelezo tofauti juu ya hali hii. kutokana na hamasa ya upigaji kura ilivyokuwa mwaka huu ni wazi kwamba watu wengi waliojiandikisha walipiga kura. watu walihamasishana sana. kwa hivo nashawishika kuhisi kwamba Tume ya Uchaguzi iliandikisha mamluki wengi sana ili CCM ije kuwatumia kupiga kura hewa. Wananchi walivodhibiti uchakachuaji, basi wapiga kura hao hewa ndio hawakupiga kura. ndiyo maana pia hata idadi ya waliojiandikisha 19 millioni ilitia shaka tangu awali