Walioshindwa maisha mjini tukutane hapa

"Bado wako hai" ndio utata, ulitakaje kwa kusema bado wapo hai?
wote hawajafa, wangekufa wote au mmoja huenda mzigo wa kuwahudumia ungepungua, au?..., haha, ndiyo maana ninahoji kuhusu uwelewa wako mkuu.
 
wote hawajafa, wangekufa wote au mmoja huenda mzigo wa kuwahudumia ungepungua, au?..., haha, ndiyo maana ninahoji kuhusu uwelewa wako mkuu.
Nimeelewa unatamani wangeshakufa ingekuwa nafuu kwako, sijakosea.
 
Mimi nilikuwa fundi rangi lakini sasa kazi za kupaka rangi zimepungua Sana, nina mke, watoto wawili na wazazi wote wako hai wananitegemea. Kodi ya chumba, chakula na maji na umeme vimeninda.

Nifanye kazi gani ingine au nirudi kijijini nilikotoka?
tatizo umewaita vipofu wenzako tu, maandiko yanasema kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake, ulitakiwa kuwaita na mapapaaa waje kusaidia.
 
Hilo ndilo balaa kabisaa, "mpemba" na rafiki zangu wenye ahueni kifedha wanaitumia hali yangu kumnyapia wife. Nikitoka kuhangaika huko na huko wao wanahamia kwa shemeji yao kumjaza ujinga. Naona iko siku tutakufa kwa maradhi
Dunia ndo ilivyo mkuu, pambana tu hakuna jinsi, kuna vijana wanauza machungwa maeneo yenye watu wengi, naona wanauza sana tu.
 
Fanya kazi/biashara zingine almradi ziwe ni za halali.
 
fanyia kazi wazo lako la mwisho hapa
kuna mwenzangu alirudi nyumbani mwaka jana baada ya kuambiwa mihogo imepatiwa soko la uhakika na Mkuu wa Wilaya, akaenda kulima eka 3 za mihogo, sasa hivi mihogo iko tayari lakini soko hakuna. Anawaza afanye nini tena na mtaji hana. Ameniogopesha.
 
tatizo umewaita vipofu wenzako tu, maandiko yanasema kipofu hawezi kumuongoza kipofu mwenzake, ulitakiwa kuwaita na mapapaaa waje kusaidia.
Nyumbani kwetu walipojua kwamba niko mjini nikaozeshwa mwanamke mzuri sana, hao mapapaa wakimuona haitakuwa shida?
 
Dunia ndo ilivyo mkuu, pambana tu hakuna jinsi, kuna vijana wanauza machungwa maeneo yenye watu wengi, naona wanauza sana tu.
Nilijaribu kuanzisha mradi wa kuuza matikitimaji ya kukata vipande, lakini kijana wangu wa kazi alilipwa noti bandia ya sh. 10,000 na kurudisha chenchi halali na mtaji umekufa kabisa.
 
Na bado Jiwe ana zaidi ya miaka 6 from now.Watu watanyooka.Na kwa mwendo huu ikifika 2025 anaeza kugoma kutoka kama kina Nkurunziza.Kuna watu mpaka muda huo wasipojiongeza watakua hoi
Nina kaeneo kangu sehemu nilikuwa na mtindo wa kuweka watu wanisafishie,siku hizi Huwa naenda mwenyewe weekend na familia nasafisha.Siweki kibarua
 
Nilijaribu kuanzisha mradi wa kuuza matikitimaji ya kukata vipande, lakini kijana wangu wa kazi alilipwa noti bandia ya sh. 10,000 na kurudisha chenchi halali na mtaji umekufa kabisa.
Daaah pole sana mkuu, hizo ndo changamoto za biashara, kikubwa ni kupambana tu hapo hapo ulipo maana ukisema urudi kijijini uje kuanza moja nako ndo kugumu balaa na kibaya zaidi utakata tamaa tu kwa jinsi wale ulowaacha kitambo walivyopiga hatua za kimaendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…