Waliosoma fani za kilimo na mifugo na Jinsi walivyotumia elimu zao mpaka sasa kujikomboa binafsi na kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo na mifugo

Hatari kubwa hiyo
 
Diploma in General Agriculture Niko zangu bandari nabeba mizigo(ila sio kuli) tafuteni Jina lingine zuri zuri kidogo. Kama Wale wanaobeba mizuho kupandisha milimani wanaitwa porters
 
Ikiwa wataalamu wa kilimo hawana umuhimu,mbona kukitokea mlipuko wa magonjwa km vile Sumu kuvu kwenye mazao au wadudu km vile Viwavi jeshi vamizi huwa mnawasumbua wataalamu wa kilimo kuwa wasaidie kutatua changamoto hiyo?,

Kunapotokea mabadiliko ya hewa hata kutishia upungufu wa chakula kwanini huwa mnawabwatukia wataalamu wa kilimo kuwa wazalishe mbegu zinazovumia Ukame au mbegu stahimilivu,si mzalishe wenyewe?.Kukitokea shida kwenye Ufanisi wa Ubora wa Viuatilifu au mbolea mbona huwa mnatoa maagizo kibao kuwa Wataalamu Wa kilimo wachunguze,si mchunguze wenyewe?.

Ikiwa hawana mchango wowote ktk Jamii Serikali inawaajiri wa nini sasa,si waache?.Jamani mnyonge mnyongeni,haki yake mpatieni".
 
Je unahitaji kulima mahindi na hauna muda wa kusimamia? Au unataka upate mavuno mengi zaidi? Njoo ofisini kwetu.

Ofisi ya YAD yenye wataalamu wabobezi wa kilimo sasa inakuletea mpango wa kusimamia shughuli zote za shambani. Mkulima utatukabidhi shughuli zako pale shambani kwako sisi tutafanya kila kitu kwa utaalamu zaidi na kukukabidhi mazao yako yakiwa yamekomaa. Gharama zetu ni nafuu sana na tunakuhakikishia kwa ekari moja kuvuna mahindi zaidi ya gunia 30. Usihangaike sasa, sisi tupo kwa ajili yako, Kwa Wale ambao hawana mashamba tutakuwezesha kupata mashamba ya kukodi kwa elfu 40 tu na mashamba ya kununua kwa elfu 60 tu hata ukihitaji ekari 100 za kununua utazipata kwa bei hiyo hiyo.

Kwa maelezo zaidi fika ofisini kwetu.
Jengo la NSSF SONGEA
Ghorofa ya 3 chumba no. 317
Simu. 0621133117
 
Nilisoma Bsc. Animal Science class of 2016 hapo SUA
Nafuga ng'ombe, kuku wa mayai(layers) na kienyeji (kuchi)
Kuhusu mtaji nilijibana kwenye boom
Karibu shambani
Congratulations Sana Kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…