Waliosoma Musoma technical high school

Hivi yule mpishi mama helena yupo?nilikua mkazi wa shabani robert domitory.
 
Tupo wengi wa enzi hizo. Pamoja na uliowataja nawakumbuka pia Muganda, Mathias, Begashe, Kituka, Gikondo. Pia kuna wanafunzi kama Ansbert Mgamba, Diocles Rutahindurwa na Simon Odunga

Kituka ni marehem (hakuwa mwalim bali storekeeper) kweli Mkuu mambo ya RPM kipindi kile utakumbuka. Pia Mwl. Malalika alinifundisha history nikapiga Banda hatari NECTA, nikamtunuku kupitumia id hii hapa jamvini.
 
Nimemaliza hapo Advance 2011 enzi za Dobeye. Namkumbuka kwa misemo yake ya ajabu ajabu. Pia nilikuwa Katibu wa Dom la Mkwawa.
 
Mi naitwa David William, nimemaliza advanced level musoma technical secondary school 2010, nilikuwa nikiishi bweni la amri abeid.

Ha ha ha! hilo lilikuwa bweni langu! kulikuwa na toilet pembeni yake mtu ukiingia unaacha shati nje! Mbali na hapo ukiingia darasani kila mtu utasikia "nani katoka magharibi jamani" maana hiyo harufu ha ha ha! Ni product ya A level year 2000! Namkumbuka mwalimu wangu wa Geography - Mwl. Amos!
 
mwaka 99 nakumbuka tulienda kucheza mpira baada ya mechi ikazuka vurugu kubwa sana,tuliwakimbiza sana mara sec na vurugu ziliendelea njia nzima na kuna magari yalivunjwa vioo njiani.....usiku zilikuja defender mbili kuja kuwakamata wanafunzi lkn nao wakapigwa mawe walipofika shuleni......basi siku hiyo palipigwa sana mabomu ya machozi na wanafunzi tulikimbilia milimani hadi asbh....enzi hizo katibu mwita magessa.....!watu walipinda sana kipindi kile.
 

Duuh... au ndoo maana mapolisi huwa wanajaa uwanjani... kwenye gemu ls teki & mara
 
Aid
Kwenda kuvinjari MAKONDEKO,kunya SERENA,free pass kwenye msosi na kukumbana na wapishi akina mzee Sabato na Matogolo,mademu wa Songe sec.walikuwa halali yetu,n.k.Ila moshi wa Mutex ulitutesa!!!

Aisee umenikumbusha mbali. Kuna wale watoto wanaitwa waloko, walikuwa wanatoa maji ya kuoshea vyombo.
 
Musoma Technical University of Mara. Mimi nilikuwepo kipindi Cha musagasa na baadae preamble.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…