Waliosoma popatlal miaka ya 1990 mpaka 1994 mpo wapi? Tuwasiliane.

magaka Makoye

Member
Joined
Sep 11, 2011
Posts
5
Reaction score
2
Wakuu leo napenda kutumia jukwaa hili kuomba mawasiliano na watu waliosoma shule ya sekondari ya Popatlal iliyoko Tanga. Kwa atakayeliona tangazo hili aache namba yake ya simu au barua pepe. Nakumbuka sana enzi hizo mkuu wa shule bwana K.R. CHAUDRI na walimu wengine kama vile Mrs Swai (mwalimu wa Kemia) Mr Muchunguzi (mwalimu wa Jiografia). Mr.Nandoli (marehemu-mwalimu wa Book-keeping), Mr. Khalid (mwalimu wa Hisabati) na wengineo wengi sana. Nimekumbuka sana mpaka machozi yananitoka kwa kuwa sina hakika kama niliosoma nao wote bado wako hai, mfano Issa Omary Issa-Almuhsin, Urasa Moses Nanyaro, Kimera Kiangi, Shaaban Kilamla,Saad Kimangare, Hamisi Kiluwasha, Suleiman Chombo, Edward Kavishe nk.
Nawapenda sana jamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…