Mimi nimekuwa nikifuatilia maandamano ya hawa wanafunzi wa vyuo vikuu na nikagundua kuna matatizo makubwa ambayo watu hawayaongelei. Gharama za kumsomesha mwanafunzi mmoja hadi kumaliza shule ni TSH 15,000,000. Tatizo ni kwamba tuna system ambayo serikali haidai pesa baada ya wanafunzi kumaliza shule na hivyo kuchukulia posho kama msaada badala ya mikopo. Shule si bure na wanafunzi inabidi wajue hivyo lakini serikali vilevile inabidi ijue kwamba kutokukusanja madeni si tatizo la wanafunzi wa sasa bali ni tatizo ya serikali kutokana na kushidwa kukusanja au hata kufuatilia madeni. Tuanze na raisi wetu je amelipa deni lake la chuo?? inabidi tuwe na system ambayo watu wanalipa madeni ya shule. Mimi binafsi nina deni hapa marekani la $38,000 na ninalipa $156 kila mwezi kwa miaka 20. Nikipanga kulipa mapema ni sawa lakini si bure na siwezi kukimbia deni kwasababu serikali itakuja kwa mwajiri wangu na kuchukua pesa kila mwezi.