TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,584
Habari Wadau!
Repoti ya CAG imemchafua sana Hayati JPM na kwa kuwa kashakufa hana pa kujitetea wapo tunaotamani hata tukamfufue ili aje kumjibu Kicheree.
Lakini sasa hayupo hata tukimtuhumu ni kazi bure, tunajichumia wenyewe dhambi na malipo ya dhambi ni hapa hapa duniani.
Ila sasa kwa waliobaki ambao wanatuhumiwa kwa upigaji wananchi tunataka rais awachukulie hatua warudishe pesa walizokwapua za walipa kodi ili twende sawa.
Itakuwa haina maana kama CAG analeta repoti nzito kama hii harafu serikali na Bunge linakaa kimya pasipo kuchukua maamuzi yeyote.
Kama kweli mama anataka kuaminika kwa watanzania basi swala la kuchukulia uzito repoti ya CAG ni muhimu.
Najua wengine washaanza kuzunguka kwa mafundi ili kupiga tunguli kumsahaulisha mama asichukue maamuzi, naomba watanzania tumuombee sana mama yetu maana kazi ya urais si kazi ndogo ni mzigo mkubwa sana.