Waliotegemea malipo ya uzeeni ujanani sasa tena basi! Ufafanuzi kutoka Mamlaka - SSRA

Kama lilipitishwa hili haki haijatendeka kabisa,Kwakua sheria ilipitishwa(01 July 2012,Kama ni kweli),inabidi michango yangu ya June kurudi nyuma niipate yote otherwise CCM itakua imejiondoa madarakani smoothly,Wabunge wa Chadema tunaomba ufafanuzi kutoka kwenu ni kweli mlilipitisha hili? Kama CCM ndio waliopitisha kwakua wapo wengi,Tunaomba 2015 Tuwaingize IKULU kwa Sharti la kuifuta hii sheria,tunawahakikishia tutawapa wabunge wa kutosha!!
 
mtoa mada,mbona sijaona kipengele cha mtu akifa je mafao yake yanakwenda wapi? ni heri niache kazi kwan jasho langu walilo-save latosha. i wish!

nadhani kama mtu amefariki zitafuata taratibu za kawaida atabenefit your next of kin ambaye ulimchagua wakati wa kujaza form zao
 
Huu utakuwa ni ujinga. Unaacha kazi kwa kutegemea 20% ya contributions zako ndio uendelezee kampuni!!!

Hii sheria ya SSRA nimeipenda. Itasaidia sustainability ya mifuko yetu na pia wanaweza kuplan vizuri especially kwenye long term investmennts.
Ndo matatizo ya kuishia darasa la pili hayo. Kizazi cha sasa sio cha kufanya kazi miaka 60 na kuwabania nafasi vijana wanaotoka shule. Mtu mwenye akili ya kijasiria mali muda wake wa kufanya kazi hauzidi miaka 10 then anaingia kuInvest kile alichopata na kutengeneza ajira kwa watu wengine. Tatizo nchi hii mnapokaa chini na kufikiria kuhusu mfanyakazi mnafikiri ni yule wa serikalini mwenye mshahara wa laki 4 kama wewe Rejao ambaye utahangaika na ajira maisha yako yote. Kuna watu wanalipwa 8 digit salary wakifanya kazi miaka mitano wanakuwa tayari kutumia ujuzi waliopata kazini kujiajiri na kuendeleza uchumi. Nyie wafanyakazi wa serikalini na vimishahara vyenu vidogo ni watu wa kuajiriwa milele, na hata kazi zenu haziwaendelezi kiujuzi kujiajiri, mfano askari polisi au takukuru atajiajiri katika kazi zipi kwa ujuzi aliojipatia kupitia kazi yake? Haiwezekani kamwe! Watunga sheria na sera lazima wafikirie in 3 Dimensions sio kuishia kwa wafanyakazi wanaotegemea rushwa na ufisadi waa serikali
 
Reactions: rom
Ccm wamechota ela zote kwenye hiyo mifuko ya jamii, na sasa hiko hoi, ili kuzuia isi-collapse ndio wanatunga sheria ya kipuuzi kama hii...
 
Teh teh teh ....kwa huo mshahara wa laki nne but nina maisha mazuri yasiyo na stress, silii lii ovyo. Kati yangu mimi na Wewe unayelipwa 8 digits halafu unaja lilia hapa nani mwenye afadhali?
 
Wewe ndio kiazi! Formula za kukokotoa mafao zimeconsider time value of money, inflation na interest! Miaka 20 ijayo utapa present value ya hiyo milion 10 yako!
 
Nimtafakari kwa umakini sana na kugundua suala hili linatakiwa lifanyiwe marekebisho ya haraka sana kulingana na life span ya mtanzania na hili suala haviendani hata kidogo kiu kweli kuna jambo mnatuficha
1.Mmeshirikisha wafanyakazi wangapi,na ni lini? Mnataka kuzidisha umasikini kwa watanzania na ubabe wenu hili jambo litatugawa nina uhakika 100% ntajutia!kila mfanyakazi amesikitika kwa sheria hii ya kipumbavu nimechukia sana hata kama mode atanipiga ban potelea mbali huu uzi ni habari mbaya sanaaaaaaa kwa sisi wafanyakazi!
 
Wamechota pesa zote sasa wanataka kubebesha mzigo wananchi, wamewakopesha matajiri wakubwa ambao hawachangii mfuko wakati wachangiaji wenyewe hawafaidiki na chochote wakati huu, wanataka wakakope kwenye mabank ambayo riba zao ni kubwa... wanatafuta laana waliopitisha hiyo sheria
 

Jamani mnashangaa hilo la mafao ya kujitoa! je, mnajua wale watakao staafu miaka 55 hadi 60 watapata nini? formula itababadilika, ile ya PSPF na LAPF iliyokuwa the best itachakachuliwa iwe sawa na ile weak ya PPF or worse! all is not well on this aspect! trade unions wamelala fofo!
 
Waraka wa SSRA ni uhuni mtupu,sitaki kuamini mambo yasiyo na utaratibu,SSRA inaratibu shughuri za mifuko ya jamii na mahusiano yote ya kisera na utaratibu yanafantwa kati ya SSRA na mifuko husika. Iweje SSRA itoe maagizo kwa waajiri badala ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo inawajibika kwake,Hapa kuna delay trick inachezwa ili wanachama wamifuko ya hifadhi za jamii wasitoe fedha zao mapema.Toka juzi nimepost tetesi kuhusiana na hili,ina maana jf kuna majuha watupu? hakuna hata mmoja aliyesikia tamko la serikali kuhusiana na hili? wapi muswada huu umepita?kama ni sheria ya APRIL 2012, imesainiwa lini mbona maamuzi yawe ya ghafla hata kabla ya taarifa kutoka kwanye gazeti la serikali.WATANZANIA TUSILALE HIZI PESA ZETU WENYEWE.MWENYE TAARIFA KUTOKA MJENGONI JUU YA HILI AWEKE WAZI
 
me nilipanga kuacha kazi pale michango yangu inapofika 15 mil. na hii inatimia mwakan nikiwa nia ni kuchukua hiyo pesa na kuanza kuendeleza biashara zangu.
nikiwa kijana wa miaka 30 sijatendewa haki kusubiri another 25 yrs. what if i didnt make it?

That's why a Government is a bunch of robbers mkuu..watu wanakufa kila siku kwa ajali,wakiwa na umri mdogo,..kwanza ukiwa 55 hata huwezi kuiinjoi hiyo pesa,..ila watafanyaje na hela zenyewe ndiyo zinaliwa kupitia kwa mashirika kama kiwira na kadhalika??
 
Hansard ya kikao cha bunge. Sasa hayo maneno yanayotamka fao la kujitoa limesitishwa mbona hatuyaoni? SSRA wasanii fulani (wametokea "wengi wao" PPF -- CEO alikuwa manager wa investment) bado ana uchu wa ku-invest hela zetu za wafanyakazi ktk miradi isiyokuwa na "returns" nzuri. Wabunge wote (chadema na ccm) wanafikiri..... (maneno ya meya fulani)....
 
Yani miaka 35 ijayo?acha nikomae na maisha kimpango wangu.
 
Teh teh teh ....kwa huo mshahara wa laki nne but nina maisha mazuri yasiyo na stress, silii lii ovyo. Kati yangu mimi na Wewe unayelipwa 8 digits halafu unaja lilia hapa nani mwenye afadhali?

lazima utakuwa fisadi wewe ndio maana unapindisha ukweli..hiyo nyumba yenyewe laki 4 haitoshi.....
 
Mi Akili yangu imegota hapa sasaa!ina maana kutakuwa na unemployment allowance kwa wale watakaokuwa wamesimamishwa kazi wakiwa katika kipindi hich cha mpito wakati wa kutafuta ajira mpya. maana kama tumecopy na kupest kutoka kwa wenzetu basi tucopy kila kitu si kutesa wananchi wafanyakazi kwa kuwanyang'anya haki yao ya msingi.
 
Ila kiukweli wabunge wetu wanatuangusha hawaoni mbali. kwa kuwa wengi tayari wamefikisha huo umri basi wanadhani kila mtu mzee kama wao. Wnapaswa kwenda na wakati na si kuturudisha walikotoka utakuta kibabu ama kibibi kizima kimepanga ati alikuwa anasubiri vimafao vya uzeeni ndo ajenge. Maisha ya leo ni kujiwekezea ungali bado una nguvu naona hawa wabunge wetu pamoja na huyo kibaraka wa serika SSRA hawasomi habari za nyakati wana mtazamo wa kizamani sana. kwakweli wameniboa sana
 
Naomba mwenye taarifa za hii mikopo atueleze jinsi ya kuipata.

Haisaidii...........nyumba ya kukopeshwa inaanzia 40m sasa ni wangapi wenye michango kama hiyo? Na je kwani wanachama wote wana shida ya nyumba? Vipi kama nataka kutumia michango yangu kama mtaji wa kujijasiria mali?
 
Hakyamungu Tunaelekea kubaya kabsaaaaa watu tunamalengo yetu kwe nye maisha wana, uhakika gani tutafika miaka 55?
Wanatuhujumu tuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…