Waliotoa Kibali cha kuua Mamba Mkubwa Duniani wafikishwe Mahakamani

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina amesema kuwa anaamini kuuawa kwa mamba aliyedaiwa kuwa mkubwa zaidi duniani ni njama na uhujumu uliofanywa na watumishi wasio waaminifu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mpina amesema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya wizara tajwa kwa mwaka 2024/2025 ambapo amehoji kwanini wizara haikuona umuhimu wa kumhifadhi mamba huyo na kuwa kivutio cha utalii.

Ameisihi Serikali kuunda kamati ya uchunguzi itakayofuatilia tukio hilo na wale wote waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria.
 
View attachment 3008227
Aisee Mkuu Figa upoo? Ukraine vs Urusi hatuisikii tena.(ni nje ya mada lakini).
1. Wahenga walisemaga "Yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yatakayokuja." Huyo mamba ameshakufa na hawezi tena kuwepo. Hoja inakuja kwamba Je, alikuwa ni huyo mmoja tu peke yake? Ninaamini watakuwepo na wengine. La msingi hapo ni kuweka sheria au utaratibu ili mamba wasiuawe hovyo bila kuzingatia taratibu zitakazowekwa.
2. Ikumbukwe kwamba huyo aliyemwuUa huyo mamba pichani, alifuata taratibu zote husika. Kumpeleka mahakamani ni kumsumbua pasipo na sababu yeyote na italeta picha ya kwamba sisi waTz ni vigeugeu- taratibu tunaziweka wenyewe halafu tena tunakimbilia mahakamani inapobainika kwamba sheria ilikuwa na mapungufu (loop holes).
 
Hivi sheria ya utalii wa kuwinda imefutwa?
Nijuavyo kuna ruhusa ya kuwinda kwa vibali maalum ambavyo muwindaji anaruhusiwa kuwinda wanyama elekezi kwa malipo.
Kama sheria hiyo imefutwa nisahihishwe
 
Huyu mrefu kuliko wote duniani wamekosea kuruhusu awindwe.
 
Haijafutwa bali imeboreshwa zaidi - sasa unaweza kumchukua mnyama akiwa hai na ukaondoka naye.
 
Huyu mrefu kuliko wote duniani wamekosea kuruhusu awindwe.
Hakuna muhifadhi anayejua urefu mamba kabla hajawindwa.
Tanzania ina mamba wengi mno kwenye hifadhi zake na hasa Nyerere National Park na Katavi kuwawinda ni sehemu ya kuwavuna ili kupunguza madhara kwa jamii nyingine za wanyama akiwemo binadamu.
 
Back
Top Bottom