Waliotumia M-Gas au huduma kama hiyo walete mrejesho

Waliotumia M-Gas au huduma kama hiyo walete mrejesho

Islam005

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2008
Posts
3,354
Reaction score
3,623
Habari wakuu,

Kuna hawa jamaa wa M-gas wanakopesha gesi kwa elf 30 tu kisha unakuwa unajinunulia gesi kwa matumizi yako. Wanasema hata ukiwa na buku tu unapata gesi.

Waliotumia tunaomba kujua faida na changamoto zake. Mfano, hiyo gesi ya buku unaweza kufanyia chochote? Je, unaweza kununua hata usiku wa manane? Etc.

NB: Ambao bado hamjatumia tuwe wapole sio kujaza uzi na blah blah
 
Lengo lake ni ili uweze kupata gesi hata ya bei ndogo ukiwa huna pesa ya kununua mtungi mzima, hivyo hata buku unapata gesi ya kupikia.

Hasara, Hiyo nunua kidogo kidogo unatumia gharama kubwa karibia sawa na mitungi 2! Ukinunua mtungi mzima unaweza kukaa mwezi hadi miezi karibia 2 wakati kununua kidogo kidogo ndani ya wiki 2 ni gharama ya mtungi. Shortly wanapiga wasiopiga hesabu vizuri na kupumbazwa na gesi za buku buku.
 
Upuuzi tu. Gesi ukilipia 50,000 mtungi mkubwa ule ukawa makini na matumizi yako inakaa hadi miezi 3. Why sasa uhangaike na buku buku hizo?!

Hizo ni akili za kimasikini ambazo watanzania wanabebelea kwenye vichwa vyao.

Tafuta gesi mtungi mkubwa jaza, nunua pressure cooker ya umeme, na Mkaa kiroba kidogo kile cha 20,000 ,friji kubwa (usichukue za mtumba, nunua za dukani brand imara kama Beko, Mr. Uk, LG, Hitachi etc),chukua na tule tufreezer tudogo. Basi. Utapunguza gharama kubwa sana kuanzia eneo la chakula, nishati na bajeti yako utaona inakwenda vema sana. Wewe ni kukazana tu kupambana maisha katika utafutaji.
 
Back
Top Bottom