Waliougua/ wanaougua tukutane

proton pump

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
6,814
Reaction score
10,104
Hello!! Wanajamvi habari ya mda huu.....

Kwa wale waliougua vidonda vya tumbo wakapona naomba tujuzane aina ya dawa ulizotumia tafadhali kwa sababu ni vidonda vinasumbua sana hata shughuli nyingine unashindwa kufanya kwa ufanisi kutokana na maumivu

Na wale ambao wanaendelea kuugua naomba tujuzane na umeugua kwa mda gani sasa

Kiukweli ugonjwa huu unapona kulingana na mazingira uliopo na sababu za ugonjwa huo kutokana na maelezo ya daktari.

Ugonjwa huu huweza kusababishwa na msongo wa mawazo kutokana na mihangaiko ya maisha ambapo mtu hupiliza au husahau mda wa kula,bacteria(pylori helcobactery).

Japokuwa kuna dawa za hospitali huwa hazina matokeo mazuri kama zile za kienyeji

Kiukweli mimi niliugua kwa mda wa miezi sita nikiwa nahangaika huku na huko kutafuta dawa baadae nikawa najaribu kila aina ya dawa.Iliyoniponesha mimi bila uchoyo ni ASALI mbichi NA KEMOXYL ambapo kemoxyl ni amoxicillin inayouzwa maduka ya dawa baridi.

Asante na MUNGU awabariki.
 
Ila Omeprazole umekula sana.
Mimi nimesumbuliwa na tumbo kwa muda mrefu, ila nimepona sasa kwa kufuata kanuni za kula vizuri, nimeacha artificial food and drink yaani kitu kama hajakiumba Mungu hakipiti kinywani mwangu, tumbo nilikuwa nalipoza kwa kuli neutralize na Bicarbonate of soda nusu kijiko kwa siku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante ndg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bicarbonate ndo nini mkuu ufafanuzi kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niliamini kwa kujiombea mwenyewe, nikakiri uponyaji kwa kutumia vile ambavyo sikuwa navitumia. Kwa imani hiyo Mungu aliniponya, ni mzima kabisa.

Mungu akuponye.
 
jino linanisumbua (molar tooth )
 
Mpaka ukajiita proton pump ilikuwaje mkuu vidonda vile tatizo kwako!!!

Tiba halisi ni vyakula na life style. Najua hapo unaufahamu namna ya ulaji mzuri kama ni mgonjwa wa muda mrefu.

Mi mwenyewe nimekuwa na vidonda miaka sasa, ila ni muda sasa havinisumbui na situmii dawa yoyote, labda mara moja moja nikikaa njaa muda mrefu, nikiwa stressed au baadhi ya aina za dagaa nikila, ambapo huwa haichukui siku nakuwa sawa.

So, nakushauri, huko uliko tafuta mtaalamu wa lishe, nenda hata hospitali kuelekezwa namna gani mgonjwa wa vidonda vya tumbo aishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli ndg nasikia kuna aina ya kundi LA damu linasumbuliwa na vidonda vya tumbo kwan sana yaani miili yao inatoa asidi nyingi hasa wale blood group O

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie niliugua kwa muda wa miezi mitatu na nilikula vyakula vyakula nilivyoruhusiwa ikiwemo maharage ya soya, kusali pamoja na dozi zao japo nimezisahau majina yao...ila kwa kifupi, ni Mungu aliyeniponya maana kama dozi sikuwa nameza kwa muda muafaka na muda mwingine napiga gap.
 
Vizur

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…