Waliowahi kufika DRC (Congo Kinshasa)

Waliowahi kufika DRC (Congo Kinshasa)

snochet

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Posts
1,433
Reaction score
1,176
Habari wadau,

Recently nimepata kimuhemuhe cha kutaka kutembelea DRC(sio kwa biashara ila ni kwa ajili ya utalii uchwara)

Nifanye road trip mpaka nitokee upande wa pili wa nchi kule kwenye bahari ya Atlantic.

Kuna mtu humu amewahi fanya hii kitu?

Experience ikoje?

Nafahamu fika kwamba Cogo sio sehemu salama sana,lakini bado natamani kujaribu culture yao kwa muda.

Naomba updates.

Asante
 
Acha kumdanganya mwenzio mkuu, wakati we mwenyewe kwa majibu ya Leo pale mahakamani unajua umeacha hakimu anaandaa mkeka wa Mvua[emoji28][emoji28][emoji28](avater yako)
Mi nachomoka nimfuate nand wangu
 
Road trip kwa congo ni ngumu, miundombinu ya barabara haijaunganishwa vzr(mf Lubumbashi to kinshasa).Ndio maana Congo viwanja vya ndege ni vingi sana.
Ukifika Lubumbashi (ukiingilia tunduma), chukua flight to Kinshasa
The same to ukipita Goma.
 
Asanteni kwa kunijuza na kwa ushauri.
Mambo yatakuwa sawa muda si mrefu nitaenda huko--->nitawaletea mrejesho na picha lukuki Inshaalah!
 
Barabara zao mbovu kabisa. Unaweza tumia miezi miwili kutoka Goma hadi Kinshasa. Mwezi barabarani na mwezi kwenye boti.
 
Hahaha mleta mada karibu RDC wasikutishe njoo hapa Lubumbashi tuanze safari .Mimi naelekea Kinshasa mwezi wa Tisa mwishoni

Tunaanzia Lubumbashi. Likasi lualaba tunapasua kati. Pale hadi Kisangani in road trip ..tunakatiaha central yote kisha tunaingia Kinshasa then equatorial province. Matandi port. .then were unaenda Brazzaville ..mm nabaki pale kamanyola
 
Asanteni kwa kunijuza na kwa ushauri.
Mambo yatakuwa sawa muda si mrefu nitaenda huko--->nitawaletea mrejesho na picha lukuki Inshaalah!
Njoo Lubumbashi sehemu inaitwa kabila avenue uliza ofc za Ruashi au SNCC then uliza code name afande ..tuonane tupange hii tour vzr
 
Habari wadau,

Recently nimepata kimuhemuhe cha kutaka kutembelea DRC(sio kwa biashara ila ni kwa ajili ya utalii uchwara)

Nifanye road trip mpaka nitokee upande wa pili wa nchi kule kwenye bahari ya Atlantic.

Kuna mtu humu amewahi fanya hii kitu?

Experience ikoje?

Nafahamu fika kwamba Cogo sio sehemu salama sana,lakini bado natamani kujaribu culture yao kwa muda.

Naomba updates.

Asante
Kkkkkk. Tafuta nchi nyingine. Hakuna barabara itakayokufikisha kule ukiwa na ari na hamu ya uamuzi ambao utaujutia maisha yako yote. Ni rahisi kutoka Dar hadi Cairo mara tatu kuliko kwenda hadi Kinshasa. Hata ukitumia ndege, ni matatizo. Ndege zao nyingi za kirusi ni za zamani na zinajazwa kupita kiasi. Kusema ukweli, heri ufikirie hata kwenda Afrika Kusini hata Zimbabwe kuliko DRC. Usipoamini ushauri huu, utaukumbuka baada ya kuanza safari yako.
 
Back
Top Bottom