Sijafahamu Kwa wengine ikiwa hupata haki Kweli kunapotokea shida za kiajira/kikazi katika nchi za kigeni, lakini hii imekuwa ni kinyume kabisa Kwa balozi zetu zilizoko Abdhabi,
Mwaka 2016, Mzee mmoja Kwa majina yake akiitwa Kwa Jina, naliweka (Kapuni) ni Mtanzania, alibahatika kupata Kazi katika nchi za UAE kama Capten wa meli akitokea Tanzania na ni mtanzania, na meli aliyokuwa akifanya, ikiitwa Kwa Jina la BLUE NILE Kampuni nimeisahau,
Mzee Yule aliingia Mkataba wa mwaka mzima na Kampuni hiyo, cha ajabu ilikuja kuonekana kwamba, hiyo Kampuni inamadeni kibao, ilitaka kuingia mfilusi ikabaki na meli moja hiyo ambayo Mzee huyo alikuwa akifanya, ktk meli hiyo walikuwa wafanya kazi wengi kutoka sehemu tofautitofauti
Mmiliki wa meli hiyo alikuaa akiitwa Mohamad Ossama, akitokea sudani, wafanya kazi hao hawakuwa wanajua kile kinaendelea kwenye Kampuni hiyo, Ila walichokuwa wakikutana nacho, ni malipo Yao kucheleweshwa na kulipwa nusu ama posho na ama hakuna kabisa, ilieenda Hadi mmiliki akawatelekeza wafanyakazi hao baharini, wakiwa hawana chochote, wakipitia Hali ngumu ya maisha, chakula hawana, basi mateso mengi, ikatokea bahati zile meli za uokozi waliiona meli hiyo ikiwa haina mwelekeo, ndipo wakapa msaada wa mafuta na hatimaye kutoka baharini Hadi bandarini
Na walipotaka kufahamu juu ya bos wao, wakadokezwa tu kuwa hayupo alishakimbia,
Bado ikabidi kila mmoja sasa aende ktk ubalozi wa nchi yake, huyo Mzee akaenda katika ubalozi wetu huko Abdhabi, Wakati huo alikuwa na Pesa kidogo za kumsafirisha kurudi nyumbani tuu,
Akiwa ubalozini, akaeleza kila kitu, ikabaki swala la ubalozi kufuatilia haki za Mzee huyo, mpaka anaondoka huko, alikuwa akiidai Kampuni hiyo $19000, na alipoliacha Hilo seals kwenye ubalozi, ni kwamba, ubalozi utafuatilia serikalini ili haki ya mtu wao ipatikane, na walimwambia watakuwa wakimpigia simu kila wiki kumjulisha kila linaloendelea huko na kumhakikishia kwamba haki yake atalipwa
Cha ajabu, alipotoka tu huko, hajawahi kupigiwa simu Wala kujulishwa kilichoendelea mpaka leo, Je, mabalozi wetu Kweli, huwa wanatoa msaada Kweli Kwa ndugu zao wanapokuwa na matatizo kwenye nchi walizopo??
Na hata Jina la aliyekuwa akifuatilia ishu Hiyo kwenye nchi hiyo, lipo na ni yupo, na Balazo wetu aliyeko huko ni mteule akitokea Zanzibar mwana mama, au walishaipata na wakaamua kuigawana, tutajuaje bhana, ikiwa hata zile ahadi za kutoa maendeleo ya ufuatiliaji wao hawakutoa??
Huyo Mzee Kwa sasa, anaomba msaada wa namna ipi atapata haki yake,
Tunaomba mchango wenu wadau