Waliowasindikiza Esther Matiko na Bulaya bungeni wafutwa uanachama wa CHADEMA

Waliowasindikiza Esther Matiko na Bulaya bungeni wafutwa uanachama wa CHADEMA

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) mkoa wa Mara kimewavua uongozi na kuwafuta uanachama wanachama wake nane akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Wilaya ya Tarime kwa kosa la kuwasindikiza waliokuwa viongozi na wanachama wa chama hicho Ester Bulaya na Esther Matiko bungeni Dodoma pamoja na kukiuka sheria za chama.

=====

Uongozi wa CHADEMA mkoani Mara umewafuta uanachama na kuwavua nyadhifa za uongozi watu nane akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wilaya ya Tarime.

CHADEMA kimefikia maamuzi hayo baada ya wanachama hao kuwasindikiza bungeni, Ester Bulaya na Esther Matiko ambao ni wabunge wa viti maalum ambao waliwahi kuwa wanaCHADEMA.

Aidha Peter Makwi ambaye alikuwa Katibu wa CHADEMA Jimbo la Tarime Mjini ametuhumiwa kuwa anajitangaza kuwa ni Katibu wa Esther Matiko ambaye hatambuliki na Chama.

CHADEMA kiliwafukuzwa uanachama wabunge 19 walioapishwa kuwa viti maalum, kwa sasa bado rufaa yao haijatolewa majibu kama wanaendelea kutambulika kama wanachama wa CHADEMA.



ITV
 
Hao ni sumu ndani ya chama, ebu endeleeni kukisafisha chama chetu kibakie kisafi.
 
Kwanini mnafukuza wa Mara hawa wa Mbeya mnawaacha?!
Unaweza hata wewe kuwafukuza. Kila mkoa unafanya maamuzi yake bila kushurutishwa na mkoa mwingine. Hawa wa Mara wanaelekea wameendelea kuwa karibu nao kisiasa hata baada ya uamuzi wa Kamati Kuu kuwafukuza kwenye chama. Labda huyo unaemzungumzia alikiri kosa na kujirekebisha baada ya uamuzi wa chama chake. Na hatakuwa peke yake kufanya hivyo maana waliofukuzwa waliaminiwa mno na chama chao. Labda walipoenda kuapa waliwaambia watu kuwa wana ridhaa ya chama au Mwenyekiti na baadhi wakawaamini.

Amandla....
 
Back
Top Bottom