IBRA wa PILI
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 1,503
- 2,426
Ilikuwa ni Oktoba 28, 1958 mjini North Carolina US ambapo watoto wa kiume wawili wenye asili ya Afrika David Simpson (na Hanover Thompson (9) raia wa Monroe walipewa kesi kwa kumtazama tuu binti wa kizungu wa umri wa miaka 7 Sissy Marcus.
Mama wa binti huyo Bernice Marcus aliwashtaki watoto hawa kwamba walimbaka kwa sura binti yake.
Mbali na shitaka hili pia waliongezewa makosa mengine ya kuwa walimlazimisha busu na kumbaka hali iliyopelekea wakae gerezani kwa zaidi ya miezi mitatu huku kwa wiki kadhaa za mwanzo wakipigwa vikali na kukatazwa kumuona ndugu yao yeyote.
Swali likaja ni wakati gani walimbusu na kumbaka binti huyo ilihali muda huo alikuwa pamoja na mama yake?
Kwa muda wote wakiwa mahabusu walipigwa na kuteswa, Polisi waliwakataza kuongea lolote, na hii ndio ikawa kama njia ya jaji Hampton Price wa mahakama ya Juvenile kutoa hukumu kwani baada ya hukumu alisema 'Kwa kuwa walinyamaza tu na hawakusema chochote, nilijua walikuwa wanakiri makosa.'
Licha ya watoto hao kuhukumiwa vifungo jela lakini walikuja kuachiwa wiki kadhaa baadaye baada ya juhudi kubwa za wapigania haki za binadamu kufanyika.
Juhudi hizi zilikuja mapema baada ya serikali kuwafukuza kazi pia wazazi wote wa watoto hawa baada tuu ya hukumu ya watoto wao kwa sababu zisizoeleweka, ikabidi pia wazazi hao wahamishiwe hadi katika eneo la mafichoni kwa usalama zaidi.
Kesi hii haina utofauti sana na kesi ya mtoto mwingine mwenye asili ya Afrika George Stinney aliyenyongwa mwaka 1944 huko US akiwa na umri wa miaka 14 kwa kosa la kusingiziwa mauaji.
Source and credit to FM fact