Acha Uvivu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 524
- 131
Bara la Afrika ni mahali ambapo matatizo ya kila sekta yanapatikana duniani. Elimu, afya, nishati, n.k zimegubikwa na matatizo lukuki, sio Tanzania, Kenya (EAC) au Ghana, Liberia (ECOWAS).
Katika kukabiliana na changamoto za sekta ya elimu kila taifa linakuja na mikakati tofauti. Tz imetambulisha Big Results Now, bila kuchanganua uhalisia (feasibility) wa mazingira ya kutekeleza sera hiyo. Maana ni copy and paste.
Maofisa elimu kila wilaya nchini wana mikakati ya kuhakikisha shule zao zinafanya vizuri katika mitihani. Moja ni kuagiza wakuu wa shule kuruhusu mitihani kuibiwa. Hii ni uhakika, usibishe. Kwa sababu lipo kisiasa zaidi (CCM) kuliko kitaaluma na mbinu za utekelezaji wake ni za kisiasa. UDANGANYIFU.
Katika nchi ya Liberia, mbali na kwamba mama Sirleaf (Rais) amejitahidi kurejesha utulivu katika taifa hilo, ukweli halina utofauti na Tanzania. Elimu inaugua sana pia.
Wao wameweka mkakati kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na chuo, lazima afanye mtihani (entrance exams). Cha ajabu wanafunzi wote 25,000 waliyotarajiwa kujiunga na vyuo wamefeli mtihani huo. "Perharps....not heard that none of the country's 25,000 university applicants passed this year's entrance exams after administrators switched to a fair admissions system based on real marks rather than bribes and family connections. Education in Liberia is a mess" Linaripoti The Ecomist, September 7-13, 2013 uk. 32.
Kilicho andikwa ktk mistari ya jarida hilo ni taswira ya kilichopo nchini, na mkakati wa Big Results Now ndo basi utaimaliza elimu Tz.
Sasa kuna vyuo Tz ambavyo vimejijengea nidhamu toka muda mrefu, kama MUHAS, Mzumbe, SUA na UD. Kama sio mwaka huu basi kuanzia mwaka kesho, waanzishe/warudishe entrance exams. Hii itakuwa ni moja ya njia kuzipiga changa la macho siasa za CCM na tume zake dhaifu za kuikwamua elimu Tz.