Waliyochaguliwa Vyuo 2013/14 Kufanya Mtihani (Entrance Exams)

Acha Uvivu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
524
Reaction score
131
Bara la Afrika ni mahali ambapo matatizo ya kila sekta yanapatikana duniani. Elimu, afya, nishati, n.k zimegubikwa na matatizo lukuki, sio Tanzania, Kenya (EAC) au Ghana, Liberia (ECOWAS).

Katika kukabiliana na changamoto za sekta ya elimu kila taifa linakuja na mikakati tofauti. Tz imetambulisha Big Results Now, bila kuchanganua uhalisia (feasibility) wa mazingira ya kutekeleza sera hiyo. Maana ni copy and paste.

Maofisa elimu kila wilaya nchini wana mikakati ya kuhakikisha shule zao zinafanya vizuri katika mitihani. Moja ni kuagiza wakuu wa shule kuruhusu mitihani kuibiwa. Hii ni uhakika, usibishe. Kwa sababu lipo kisiasa zaidi (CCM) kuliko kitaaluma na mbinu za utekelezaji wake ni za kisiasa. UDANGANYIFU.

Katika nchi ya Liberia, mbali na kwamba mama Sirleaf (Rais) amejitahidi kurejesha utulivu katika taifa hilo, ukweli halina utofauti na Tanzania. Elimu inaugua sana pia.

Wao wameweka mkakati kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na chuo, lazima afanye mtihani (entrance exams). Cha ajabu wanafunzi wote 25,000 waliyotarajiwa kujiunga na vyuo wamefeli mtihani huo. "Perharps....not heard that none of the country's 25,000 university applicants passed this year's entrance exams after administrators switched to a fair admissions system based on real marks rather than bribes and family connections. Education in Liberia is a mess" Linaripoti The Ecomist, September 7-13, 2013 uk. 32.

Kilicho andikwa ktk mistari ya jarida hilo ni taswira ya kilichopo nchini, na mkakati wa Big Results Now ndo basi utaimaliza elimu Tz.

Sasa kuna vyuo Tz ambavyo vimejijengea nidhamu toka muda mrefu, kama MUHAS, Mzumbe, SUA na UD. Kama sio mwaka huu basi kuanzia mwaka kesho, waanzishe/warudishe entrance exams. Hii itakuwa ni moja ya njia kuzipiga changa la macho siasa za CCM na tume zake dhaifu za kuikwamua elimu Tz.
 
Noumer sanaaa! Mtihan gan huoo tena after ule wa necta ACSEE!
 
Ni mtihani, ambao baada ya kufaulu NECTA, unaufanya unapojiunga na chuo kuanza muhula (semester) ya kwanza.
 
wewe uliufanyaa enzi zako?

Mbona mnatetemeka? Mimi sikufanya kwa sababu ufaulu wangu ni wa uhakika, na hapakuwa na sera inayoshawishi wizi wa mitihani.

Hoja iliyopo mezani inahusu udanganyifu katika mitihani, wizi, na kuvujisha. Na zaidi ni hatari iliyombeleni itakayotokana na Big Results Now inayowasukuma maafisa elimu na wakuu wa shule kuvujisha mitihani ili wilaya zao zionekani zimefanya vizuri.

Sasa kwa mazingira haya taifa halitakuwa na wasomi wa uhakika, na ili kuwasukuma wanafunzi wajisomee kwa maarifa lazima mitihani kama hiyo iwepo. Hii itadhibiti uchakachuaji.
 
Hili ni jambo zuri huenda kutokana na uchanga wangu silifahamu kiundani ila kiukweli litaifanya elimu yetu kua yenye hadhi na kupata wataalamu wenye sifa stahili. Liletwe na hapa tz
Inawezekana ila sijajua hili suala litasimamiwa na nani Maana Nchi yetu inashusha imani kwenye usimamizi!! Je chuo husika? Je vigezo viwekwe sawa kwa vyuo vyote? Hofu yangu ni kwamba kuna vyuo na taasisi hasa Binafsi ziko kimaslahi. Serikali itathubutu kuwanyooshea kidole?

Nionavyo-;

iwe ni sheria na isimamiwe kama sheria nyingine na isiwe option kwa chuo fulani kuamua
 
Bonge la idea watuwekee huo mtihani tuufanye na sie.
 

Ungeweka kando umbea wa kisiasa na hisia zako binafsi kisha ukazingatia mtiririko wa uandishi, pengine ungekuwa na article nzuri - kwa hivi ilivyo hakuna jipya hapo!
 

sio kwamba tunaogopa mkuu, but nina utata na hili wazo lako naona limekuja baada ya hii sera ya big result now, kwa hiyo isingekuwa sera ya big result now.., hili wazo lako nadhani usingelitoa au sio..! Na je vp kuhucu sekta zingine tofauti na elimu ambzo zipo kwenye huu mpango wa big result now nako una ushauri gani? By the way big result inaanza na watahainiwa walioko mashuleni now na sio form six waliohitimu 2013/2014..! So wazo lako zuri but tutalifanyia kazi kwa ajili ya mambo yajayoo
 

Nakupongeza kwa ulivyo changanua, lakini huenda hujapata nafasi ya kukutana na maafisa wa elimu wilaya na wakuu wa shule ukalielewa hili vizuri. Nimelileta hapa tulichanganue, na liwe mwongozo kwa kile ambacho kitafuata mbeleni maana kila mhusika ktk sera hii anasema haiwezi kufanikiwa km mazingira ya elimu yatabaki vilevile.

Tishio lipo maana kuna taarifa kuwa maafisa elimu wote wilaya wamechimbwa mkwara lazima wafanye vizuri. Nao wamekuja na mkakati wa kuvujisha ili wasije poteza maslahi yao (chanzo cha mada hii). Sasa unatarajia nini kwa watakao hitimu kuanzia 2014? Maana sera inajumuisha msingi mpaka kidato cha sita.
 


Bado hujani-convince kabisa,kwanza hii article imekaa kisiasa zaidi (kudidimiza chama tawala)...pili ni article ambayo ina mapungufu mengi;
1.haipo proved
2.full of false details
3.most of its info. are secret (intelligence)
 
Ungeweka kando umbea wa kisiasa na hisia zako binafsi kisha ukazingatia mtiririko wa uandishi, pengine ungekuwa na article nzuri - kwa hivi ilivyo hakuna jipya hapo!

Huwezi jadili mada bila chanzo kuhusishwa. Sera imetokana na CCM, kwa nini tuwakwepe?
 
Mkuu kwa kuthibitisha ufaulu wako mzuri kwa muonekano umemaliza chuo. Tuwekee transcript yako hapa kama uko chuo tuwekee matokeo yako ya semister iliyopita tuelewe huo uwezo wako.
 
UDSM walikua na system ya kufanya matriculation examination baada ya application na selection ilitokana na matokeo ya huo mtihani sijui ni lini waliachana na huo mfumo maana nakumbuka mwaka 2004 nilifanya huo mtihani...ni mtihani wa mzuri kama ile ya GRE au GCE kwa mnaoifahamu...
 
Kama kutakuwa na taratibu safi hasa wanachuo wapewe muda wa kujiandaa sio tatizo iwepo tu hiyo mitihan, maana si unajua watu wakihitimu masomo wanaingia mitaan kusaka pesa sio kujiandaa na hiyo entrace. Na kama wewe ungefaulu kimishemishe huwezi kutuambia humu, sijawah kusikia baba au mwalimu akimwambia mwanafunzi "mimi nilikuwa wa mwisho darasan mwanangu soma kwa bidii usiwe kama mimi"
Semeni ukweli bana! Wengine mlikuwa vilaza tu tena zaman umakin haukuwepo mitihan iliibwa saaaana! Acheni mbwembwe wakubwaaaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…