The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameibuka mshindi wa kiti cha ujumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaofanyika leo huko Cairo,Misri.
Karia ameshinda kwa kura nyingi za ndio kwa vile alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kuwakilisha kanda ya soka ya Baraza la vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).
Katika hatua nyingine, Rais wa Caf, Patrice Motsepe amechaguliwa kuongoza tena shirikisho hilo kwa miaka mitano ijayo baada ya kupita bila kupingwa kama mgombea pekee wa nafasi hiyo.
Motsepe ataiongoza tena Caf kwa miaka minne hadi 2029 baada ya kumaliza awamu ya kwanza iliyoanza 2021.