Walokole wenzangu, kutumia mitishamba sio uganga

Walokole wenzangu, kutumia mitishamba sio uganga

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Tumepewa roho na mwili, kwahiyo usiishi kiroho zaidi ukasahau kuwa una mwili, unatakiwa kubalance vitu hivi viwili.

Si mara moja, si mara mbili, walokole wengi wako radhi AfE kuliko kutafuna mzizi, hao hao ukiwapa vidonge wanashukuru.

Sio kwa ubora wa dawa za kizungu bali baadhi yetu wanaamini dawa za kienyeji ni ushirikina[emoji848][emoji848]

Kuna uchawi/ushirikina gana ukitafuna mzizi wa mpera kutibu tumbo?

Kuna ubaya gani ukichemsha majani ya mpapai ukanywa ukijitibu malaria?

TUMIA AKILI KWA KADRI ULIVYOPEWA
 
Wanasahau kwamba hata viazi, tangawizi nk nimizizi...😂 Wale jamaa mihua nawaona kama akilizao hazipo tamam..😎
 
Tumepewa roho na mwili, kwahiyo usiishi kiroho zaidi ukasahau kuwa una mwili, unatakiwa kubalance vitu hivi viwili..

Si mara moja, si mara mbili, walokole wengi wako radhi AfE kuliko kutafuna mzizi!! hao hao ukiwapa vidonge wanashukuru!

sio kwa ubora wa dawa za kizungu bali baadhi yetu wanaamini dawa za kienyeji ni ushirikina[emoji848][emoji848]

kuna uchawi/ushirikina gana ukitafuna mzizi wa mpera kutibu tumbo??

kuna ubaya gani ukichemsha majani ya mpapai ukanywa ukijitibu malaria??
TUMIA AKILI KWA KADRI ULIVYOPEWA
Hivi kuna mlokole nwenye akili mbona wengi wanafuata tu kama manyumbu ulokole ni cult sio kingine we fuatilia matukio yao wanao fanya kwasasa duniani.
 
Kuna mlokole alikuwa anaumwa mafua na kikohozi Hadi huruma mi nkamwambia chukua vitunguu,tangawizi limao,mdalasini na asali changanya utapona tatizo lako akasema mambo ya kiganga wamezuiwa kanisani kwao.
 
Kunahatari walokole wasiwe wakristo.


KUNA WATU WATAKUWA NA ULOKOLE KULIKO UKRISTO.


YESU ALIWAHI kuponya wagonjwa kwa udongo alifikicha udogo akawapama machoni wakaona.

Kuna maeneo ya kutumia jina la Yesu na maeneo ya kutumia Dawa.

YESU ALIMALIZA YOTE.

NAWAHURUMIA WALOKOLE MSIO WAKRISTO.
 
Walokole wanaozitumia vizuri bongo zao ni wachache mno,Hakuna tofauti kubwa sana kati ya Teja na Mkolokoke
 
WALOKOLE WENGI WANA HII TABIA.

watu Hawa huniheshimi kwa midomo Yao mioyo Yao IPO mbali na Mimi Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.


MATHAYO 15 : 8- 9
 
Tunao walokole wengi tunawatibu kwa tiba ya mitishamba.Suala la kukataa asili ni suala la mmoja mmoja, wanaojitambua wanabugia mno mitishamba.Nilikutana na mgonjww ana miaka mitatu na ugonjwa na alishaomba Mungu mpaka amekata tamaa,nikampa dawa baada ya mwezi akarudi na zawadi.
 
Back
Top Bottom