Walugaluga crew - Ingekuwa soo

Walugaluga crew - Ingekuwa soo

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
Tunaendelea tulipoishia diss track za sister p kuhusu ngoma ya mwana fa na jay moe " ingekuwa vipi.?

Leo tunakutana na clew ya " walugaluga crew " na ngoma yao inaitwa "ingekuwa soo"
Unaweza kuona kama majina hapa idea zinafanana twende kwenye maada..

Sehemu ya majibu ya Walugaluga clane
Kwa mwana Fa & jay moe ngoma inaitwa "ingekuwa soo" bila kusahau kuwa diss " wadango family & sister P..

Katika Verse ..1 Walugaluga clane watoa puch Ryhems zenye mashairi ya vijembe kwenda kwenye Crew ya wandago family. .

"Angekuwepo hai D rob/ na kaka Ramson angekuwa Bongo/ Y Thang bila kidato namrudisha K single/ kwanza ingekuwa mfano kwa ma mc wa Bongo/ na vibaka kama wadango kwenye mfuniko kwenye Udongo..

Hapa walugaluga clane wanadai " kwanza ingekuwa mfano kwa ma mc wa Bongo/ na vibaka kama wadango kwenye mfuniko kwenye Udongo..

Wana maanisha wadango family ni wezi wa idea wameiba idea ya mwana Fa na jay moe kupitia wimbo wao wa " ingekuwa vipi" na wandago family wao wakatoa nyimbo inaitwa " ingekuwa poa"

Originally version ya mwana fa & jay moe ilikuwa inasema hivi Verse..1 ( ingekuwa vipi)

Ingekuwa vipi angekuwa hai D-Rob?
Na Chief Ramso angekuwa Bongo?
Wahisani bila kidato?
Na umrudishe K-Single?

Kwanza ingekuwa mfano?
Au tayari ingekuwa chongo?
Kati ya nani angekuwa uigo?
Na nani angebaki mzigo?
Lakini pia vile vile wana toa diss kwa jay moe mara hii Walugaluga clane wanasimama ama wana mtetea Dully sykes kwa kile alichokisema Jay moe na mwana Fa katika wimbo wao unaitwa " ingekuwa vipi"

Verse ya mwana fa & jay moe hii hapa inasema..

"Mwanafalsafa: Ingekuwa vipi Dully Sykes angeimba Hardcore?
Mashairi kama Jay Mo?

Neno wanasesere n'na imani lisingekuwepo.
Mauzo ya Rap ya bongo yangefika Platinum tano

Jay moe : Mauzo ya rap ya bongo yangefika Platinum tano!

Walugaluga clane nao wakawa jibu mwana fa na jay moe kwa kusema..

"Ingekuwa poa Dully sykes angeimba Hard core/ mashairi kama jay moe hapana..?/ jay moe wanasesere na ndio maana ameimba bishoo/ we Bishoo tu / jamani hi ni nyimbo tu tusije tuona Roho.

Lakini Walugaluga clane hao hao waka engemea upande wa "wandago family " Crew ambayo ilikuwa ni sehemu ya makundi yanayounda koo ya "walumedago " na walikuwa wanaishi temeke .

Walugaluga clane wanasema..

"Ingekuwa soo maisha ya temeke yangekuwa juu kidogo/ unadhani wasanii wangejiita ma bishoo kama jay moe"

Hii verse ilitokana na kipande hiki cha mwana fa na jay moe.

Ingekuwa vipi, maisha ya Temeke yangekuwa juu kidogo?
Unadhani wasanii wangejiita walume ndago?

Jay moe : Ingekuwa vipi Bongo Records isingekuwa ya Halfani?
Watu kama flani-flani tusingewasikia hewani!

Lakini pia walugaluga clane wanaendelea kumdiss sister P na kumpa shavu zay b kuwa yenye ni. Bora kuliko sister P.

Ingekuwa soo Bongo Record nisengekuwa ya Khalifan / mtu kama sister P tusingemsikia Hewani/ lakini nature na solo tulisha wasikia zamani / Ingekuwa so kwa sister p angeendelea kumkela zay B/ kwani zay b ni dio Danger ukiendelea kumchezea atakujicha

Hii ni diss kwa sister p coz P funk majani aliimpa fursa kubwa sana sister P katika studio yake ya Bongo Record.

Kwahiyo walugaluga clane walikuwa wana amini bila msaada wa P funk majani wa kurekodi nyimbo Bongo Record msanii ama Raper sister P sio lolote sio chochote in short alionekana kama sio msanii mwenye level kubwa zaidi ya zay b enzi hizo .

Inaendelea...

( muonekano mpya wa sister p baada ya kuolewa na kuwa mama mchungaji)
1737657871687.jpg


#funguka

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
 

Attachments

  • images-73.jpg
    images-73.jpg
    26.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom